Ndugu
Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania,kupitia Ofisi ya Raisi- Tume ya mipango imeanzisha majadiliano ya Wadau kitaifa yanayohusu mchakato wa Maendeleo baada ya kufikia kipindi cha Malengo ya Milenia, mwaka 2015. Malengo ya Milenia ni makubaliano yanayozitaka nchi zote zilizoendelea na zinazoendelea kufanya kazi kwa pamoja kufanikisha malengo hayo.
Kwa kifupi Malengo ya Milenia yanayoishia mwaka 2015 yanasisitiza maendeleo katika maeneo ya afya, elimu, mazingira na ustawi wa jamii kwa ujumla.
Tanzania ni kati ya nchi zilizoitikia wito wa Malengo ya Milenia, na imefanya vizuri katika maeneo mengi, ingawaje matokeo katika baadhi ya maeneo sio ya kuridhisha.
Kwa kuwa sasa hivi tunakaribia kufikia mwisho wa Malengo ya Milenia, na kwa kuwa baadhi ya nchi bado hazielekei kuyafikia Malengo ya Milenia ifikapo 2015 kama tulivyotegemea. TAKNET inaungana na tasisi zingine kukusanya maoni yenu ili kupata vipau mbele kitaifa ili kupanga mikakati endelevu ambayo wewe miongoni mwa wadau unaamini kuwa itakuwa na ufanisi. Taarifa itakayotokana na majadiliano haya, itachangia katika kuandaa mikakati mipya na malengo mapya tunayoamini yatatoa msukumo wa kimaendeleo duniani kote, hususani katika nchi yetu.
Mjadala huu uzingatie pamoja na mambo mengine maswali yafuatayo:
a) Makundi yepi ya watu hawaishi maisha mazuri katika jamii utokayo?
b) Ni kitu gani kimeyafanya maisha ya watu kuwa mazuri au kuwa mabaya siku za karibuni, na nini unadhani kifanyike kurekebisha hali ya kutoishi maisha mazuri?
c) Kitu gani kifanyike na lini kifanyike ili kuwezesha watu kuishi maisha bora?
d) Ni nini kinahitajika ili kufanikisha hayo mapendekezo?
Mjadala huu unasimamiwa na:
Dr. Oswald Mashindano
Dr. Tausi Kida
Mrs. Margareth Nzuki
Mrs. Vivian Kazi
Mr. Abdallah Hassan |