A joint initiative by the United Nations, The Government of Tanzania and The Economic and Social Research Foundation  

A platform for professionals and experts to meet, share and exchange experiences
Username >

Password >

Forgot | Change Password? Register! Home
Topic : Msongamano wa Magari Jijini Dar Es Salaam: Nini Kifanyike?  
 

Utangulizi
Msongamano wa magari jijini Dar es Salaam unaweza kusimuliwa kwa namna nyingi. Moja ni ile ya kutazama hali ya maisha ya watu, kipato chao, elimu yao, kazi wanazofanya na sehemu wanayoishi. Ukweli ni kuwa, kila anayeishi jijini hapa ana maelezo yake ku ...Click here to read more

     
Comments From TAKNET Members
Omari Mwinyi Khamis  : Friday, June 18, 2010    
 

Ndugu zangu tukizungumzia barabara za hewani(flyovers) zijengwe ina maana gharama za kujenga baraba zitapanda juu.Kama msemavyo lazima kuwe na utafiti sio tu wa kwamba ni wapi zijengwe na nyumba gani zivunjwe bali pia itabidi ifanyike utafiti wa ujenzi kama tunavyosema kwa kiingerza-rock mechanics investigation.Uchunguzi huu ni muhimu ili hizo ”flyovers” ziwe ni za kudumu na pia kuondowa uhofu wa kuanguka.Gharama zote hizi zinaweza kuepukwa kama tungelipanga mpango wa kujenga mji mpya wa Dar es Salaam na kupanga kimakini barabara zake pana na jinsi usafiri wa uma utakuwa vipi tukitumia mabasi makubwa yenye kuchukuwa kama watu 50 kwa mpigo mmoja.

Gharama za kuujenga mji mpya wa Dar es Salaam zitoke katika mikopo ya ndani ya nchi na pia nje ya nchi.Kama serkali yetu ingelishiriki katika uchimbaji wa madini ya dhahabu kwa kuwa na asilimia kama 50 hivi katika kila kampuni ambayo inachimba dhahabu Tanzania kwa mfano Barick Gold Company basi tungelikuwa na fadha za kuujenga mji mpya wa Dar es Salaam bila ya kuomba msaada wowote.

Ndugu Maro, wakati namjibu ndugu Besha niliona hoja zako kuhusu flyovers.Hapo juu nimeandika kuhusu rock mechanics investigation.

This is the same procedure we are conducting in mines in order to prevent scaling the pillars to a minimum size and prevent collapsion.This rock mechanics investigation takes into account the pressure that a pillar can stand.Therefore flyovers will stand on pillars tah are constructed to stand the maximum pressure.Yes corruption is another problem.

You can our bridges are washed away during every rain period!This is due to bad construction and also corruption!

 

Dr.Khamis

Consultant Exploration /Geophysics/Geochemistry and Mining Geology

Sweden

 
     

Festo E. Maro  : Friday, June 18, 2010    
  Mimi ninawasiwasi sana hili wazo la kujenga "flyovers" kwa kuwa government procurement system is not corruption free zone. Flyovers needs to be of highest safety standards and has last for long period. This is important due to its architecture and possible impacts it might have if collapse. Road project constructions have been reported by CAG to lack value for money hence lack quality and leave shorter periods. Personally I will be afraid to suggest flyover because I know if constructed it will lack value for money due to corruption. A good example is our roads, nowadays it hard to see a new tarmac road to stay for two years free of potholes or its surface to be rough similar to uncovered roads. In other countries a tarmac road stays more than 10 years and still maintains its quality. I won’t be surprised to hear news about a collapsed fly over that kills hundreds if constructed in Tanzania.  
     

rm besha  : Thursday, June 17, 2010    
  asante bwana omary,kwa kiasi kidogo ninakubaliana na wewe kwenye swala la barabara za hewani (fly overs). ila ninakubaliana nawe kwa kishindo kwenye long term plan. ningependa tu kusema kwamba fly overs zitakuwa ni suluhisho kwa muda mfupi sana na nimetoa mfano hai wa kule lagos nigeria ambako wanazo hizo fly overs lakini bado hali ni tete.

kwenye swala zima la gharama, tukirudi hapa nyumbani kwetu, suluhisho pekee ni kuwa na usafiri wa umma ambao ni wa kuaminika na ambao uko synchronized(upitao kwa muda maalum). huwezi kupanua barabara wakati unaendelea kuwapa watu hamasa ya kununua magari. tunapoongelea upanuzi wa barabara au kujenga barabara za hewani kuna gharama nyingi pia, kuna kufanya tafiti za kujua kwanza ni barabara ngapi, zenye upana upi zinazoishia wapi zinaingilikaje, zinaingilika wapi, zitasababisha nyumba/majengo mangapi yavunjwe, watakaovunjiwa walipweje, n.k. hizi tafiti pamoja na ujenzi wenyewe ambao kama hautafikiria namna gani watu wataacha kuwa na tamaa ya kununua magari zitaleta mzozo mkubwa kwani baada ya miaka kadhaa tutakuwa pale pale.

ninasisitizia swala la kuwa na usafiri wa umma ambao unafanya kazi masaa ishirini na nne na ambao utapewa kipaumbele kwa kutumia nguvu ya serikali ili ratiba yake isivurugike kamwe. nchi za ulaya, usafiri wa umma unapatikana mpaka usiku wa manane, watu huenda disco na kurudi na mabasi ambayo yana muda maalum. pia usafiri huu wa umma umepewa heshima pekee kwamba kama ni treni ipitayo katikati ya barabara ya kawaida ya magari, magari hukaa pembeni ili kuipisha. zikitungwa sheria mpya za kuwezesha zoezi kama hili na tukapata mabasi ya umma ambayo hupita kwa muda maalum bila kuchelewa na yakawa na hadhi ambayo hata mwenye suti akipanda ataendelea kuheshimika, hakuna shaka wengi wetu watapaki magari nyumbani, kwa kiasi kikubwa foleni itakuwa imepungua, kutoka hapa ndio tufikirie kujenga ma-highway na fly overs ambazo zitafanya kazi kwa muda mrefu kwani watakaoona umuhimu wa kuwa na magari au wa kuendesha magari kwenda kazini watakuwa wachache.

labda huu waweza kuwa ufumbuzi wa msingi na wa gharama ambazo hazitakuwa za kutisha.

Akhsanteni.
 
     

Omari Mwinyi Khamis  : Saturday, June 12, 2010    
 

Nakubaliana nanyi kwamba Dar es Salaam (mpya) inahitaji Long –term-plans.Hii ni plan ya miaka 100 ambayo inagawanjwa kwa miaka 10 kumi.Ni plan ambayo inajaribu kutabiri si matatizo ya msongamano wa magari tu bali pia mitaro ya maji machafu na jinsi ya kuwapatia watu maji na umeme.

Ujenzi wa flyovers ni mzuri na haugharimu fedha nyingi kama utengezaji wa underground tunnels kwa ajili ya reli.Kwanza sasa hivi TRL imeshindwa na usafiri wa abiria kabisa kwa hivyo hawataweza na usafiri wa abiria wa jiji la Dar es Salaam.Jambo la pili ni kwamba mwamba wa mawe uku chini sana katika mji wa Dar es Salaam na hii itasababisha ujenzi wa underdround tunnels kugharimu fedha nyingi sana.Bali kama ukijengwa mji mpya tunaweza kupitisha reli kando au katikati ya barabara za mji ili kuweza kupitisha TRAMS kwa usafiri wa watu.Mifano kama hii iko katika miji mikubwa kadhaa kama Amsterdam na Paris.

Tumekwisha ambiwa na viongozi kwamba Dodoma hawatahamia kwa hivyo lazima tutatuwe msongamano wa Dar es Salaam.Msongamano pia huletwa na viongiozi na misafara yao.Kwa mfano Rais akituoka ikulu kwenda kiwanja cha ndege kwa nini hao wanaompangia safari wasimsafirishe kwa kutumia Helikopta?

Ringroads ni nzuri na zinatumika miji kadhaa.Pia njia kubwa katika nchi nyingine hazipiti katikati ya miji bali zimewekwa nje ya miji.Hii ni kwa sababu nje ya miji kuna maeneo makubwa ya kuweza kuzipanua njia hizi wakati zinapotakiwa kufanya hivyo bila ya kuleta ubomowaji wa majumba!

Dr.Khamis

Sweden


 

 
     

boniphace makene  : Saturday, June 12, 2010    
  Ndugu Mbesha, nakushukuru sana kwa mchango wako makini kwa awamu zote ulizochangia. Nadhani kuna jambo la kusisitiza hapa kuhusu nia njema ya kuondoa msongamano na hoja iliyopo ni kuhusu gharama. Je, tunadhani nini namna njema ya kupata fedha za kujenga Dar es Salaam mpya na pia kumudu kutanua miundombinu il kufikia lengo la kuifanya Dar kuwa sehemu bora kwa wananchi kuishi?  
     

rm besha  : Friday, June 11, 2010    
 

AWAMU YA MWISHO

Kwa kumalizia  ninaipinga hoja kwamba kuongezeka kwa magari ni maendeleo. maendeleo yahusianayo na usafiri ni ambayo yanamwezesha mtu wa kipato cha chini kabisa na mtu wa kile cha juu kabisa kuweza kutumia usafiri wa aina moja na wote wakiwa wameridhika. Maendeleo ni pale ambapo unaweza kupaki Vogue yako na kuamua kupanda basi na ukasoma gazeti lako au kufanya kazi kwenye laptop yako kwa raha mustarehe kama uko nyumbani. Usafiri ni moja ya mahitaji muhimu sana ya jamii, serikali yetu inabidi ilitambue hili na ihakikishe kuwa wakati viongozi wake “wawakilishao” wananchi masikini wanapanda VX za starehe na gharama ya hali ya juu, hao wananchi masikini “wawakilishwao” wangepandishwa kwenye usafiri  wa umma ambao angalau unakaribia kiwango cha usafiri wa viongozi wao (maana viongozi na wananchi wote ni wa humu humu Tanzania kwenye umasikini). Mabasi wayapandao wananchi ni ya kiwango cha chini kabisa kuliko usafiri wa aina yeyote hapa nchini; ninayaweka kwenye daraja moja na magari ya taka.

Si ajabu waziri wa miundombinu angenyimwa gari ya serikali na kukatazwa kupanda gari binafsi ili alazimike kupanda mabasi, angeweza kuelewa ni shida gani wazipatazo wananchi wake masikini anao“wawakilisha” na angeumiza kichwa kwa kutafuta utatuzi wa swala la usafiri wa umma ambao unaweza kupunguza adha ya msongamano hapa mjini.


ni haya kwa leo.
AKHSANTENI...

 
     

rm besha  : Friday, June 11, 2010    
 

AWAMU YA PILI

pia ulaya kuna miji mingi tu ambayo wanatumia mfumo wa ring roads. kwamba barabara za magari hazifiki ndani ya mji. zinatengenezwa sehemu za maegesho ya magari zaweza kuwa surface parking au parking towers; kwa hapa kwetu ni kwenye maeneo kama ya mbele ya royal palm kisha watu wanaingia mjini kwa miguu...hili nalo lawezekana ila tu kwa hali ya hewa yetu, kuna mambo ambayo inabidi yafanyike ili kulifanikisha, kwa mfano kupanda miti na kujenga structures ambazo zitawakinga watu jua watakapokuwa wakitembea kwa miguu kuelekea na kutoka mjini mpaka kwenye magari yao. pia gharama za kuegesha magari katikati ya mji zipandishwe kwa kiwango kinachotisha ili kwenda na gari mjini iwe ni anasa. vile vile mji usijazwe maofisi tu, wanaohusika na kuupanga wafikirie pia shughuli tofauti kama recreational spaces (sehemu za kustarehe na kupumzika), ofisi zifanywe shopping malls na migahawa, waweke gardens, ma-hoteli, maduka ya vinyago,  n.k. zile shughuli ambazo hazitahitaji magari mengi yatakayokaa muda mrefu hivyo kusababisha foleni ndio zibakie katikati ya mji.

bado tukiwa hapahapa kwenye kuupanga mji, sasa hivi ambapo kila mtu anaamua ajenge nini kwenye kiwanja chake huku kwenye makazi kama sinza, kimara, mbezi n.k., ni kipindi ambacho kimeleta msongamano mkubwa mno kwani kwenye maeneo ya makazi ya watu, kuna maofisi, kumbi za burudani, baa, kumbi za harusi, makanisa, n.k. hizi ni shughuli ambazo zinakuja na magari mengi tu pamoja na misafara ya harusi isiyo na msingi. sehemu za makazi zingebaki kama zilivyo na sehemu za starehe zikatengwa, ingeweza kusaidia.

Tatizo lingine kubwa ni misafara ya viongozi wa serikali, sifahamu kama lilishatajwa lakini ni kati ya matatizo makubwa kabisa yasababishayo msongamano mkubwa sana. Hii ni misafara ambayo huanzia na kuishia katikati ya mji ambako ndiyo kuna msongamano mkubwa kabisa. je, ikulu yaweza kuhama, au nini kifanyike kwenye hili?hapa nimekwama.


pia, lazima tufahamu kwamba wenzetu wanakuwa na long term plans, kwa mfano kwenye miundo mbinu, wanaweza kuweka miaka hata ishirini au thelathini ya kupanua barabara na kujenga reli na underground tunnels au flyovers, kupanua miundo mbinu siyo kazi ya mwaka mmoja kama tudhaniavyo. bila kuwa na vision na pia moyo wa kuwafikiria watoto na wajukuu wetu huko baadae, tutaishia kutaka kupanua barabara tu ili tuzitumie sisi wenyewe, na viongozi wetu ndivyo wafikiriavyo..na tukakuta bado tatizo ni kubwa, mfano hai uko lagos, Nigeria ambako waliamua wajenge flyovers na sasa hivi hali ni tete ambako walifikia hatua ya kuruhusu magari yenye nambari za usajili kama even na odd numbers kuwa na siku maalum ya kuendeshwa.

pia, tusitegemee sana serikali ifanye kila kitu, sababu kubwa kwanini oysterbay kuna barabara nzuri za lami ni kwamba kwanza ni makazi yaliyopangwa (formal settlements) hivyo wanalipa kodi na pia ni kwa wakubwa,na hivyo basic needs kama barabara zitajengwa na zitakarabatiwa,huku kwetu ambako hakujapangwa (informal settlements) kodi hailipwi na hivyo jicho la serikali haliangukii huko, cha msingi ni wananchi tujipange ili tuendeleze makazi yetu kwa kuziimarisha hizi barabara ziwe na kiwango cha kufaa ambacho kinaweza kuruhusu barabara hizo kutumika katika kupunguza msongamano.kama tunaweza kununua X5, Benz, VX, Lexus, Lemo na mengine mengi ya bei zaidi, tunashindwaje kujumuika na kuzibadilisha barabara kwa kutumia pesa zetu wenyewe au kwa msaada we serikali kwa namna yeyote?hii ni changamoto!

 

 
     

rm besha  : Friday, June 11, 2010    
 

ninawasalimu ndugu zangu,

ninashukuru sana kuwa mmoja wa wachangiaji kwenye mada hii ambayo ni tatizo kubwa sana. mimi napenda kuweka msisitizo kwenye mambo ambayo baadhi nyinyi wenyewe mmeshayataja ila ndio ambayo ni muhimu sana kuhusiana na swala zima la msongamano hapa DSM.kwa kuwa mchango wangu ni mrefu kidogo, nitauvunjavunja na kuutuma kwa awamu.

AWAMU YA KWANZA

kwanza, ningependa kusema kwamba mambo yanayosababisha msongamano wa magari yana uhusiano wa karibu sana; kwamba bila kuyatatua yote ambayo ni sawa na kusema tunabadilisha mfumo mzima, tutakuwa hatujafanya lolote… hii nitaielezea kwa kutaja na kujadili mambo yanayosababisha msongamano na mifano hai. Kwa kuanza , ma-trafik wetu wengi ni watu ambao hawana uzoefu wa kutosha wa ku-manage trafiki nzito kama ya dar es salaam. trafiki ambaye anakaa moroko alipaswa awe na mawasiliano na trafiki ambaye yuko mjini, na wa mwenge pia ili ajue anaruhusu gari zipi ziende wakati nyingine zikisubiri. Kwa kifuoi tu ni kwamba kwa ufinyu wa barabara zetu nyingi an kwa wingi wa magari, ilipaswa kuwe na mfumo au network maalum ya jinsi ya kuyaongoza magari hapa mjini. Hii ni network ambayo ingeweka bayana barabara ipi inachukua magari mangapi muda gani na lini maana mzunguko wa magari ni ule ule, hii ingeweza kutoa utatuzi mbadala wa kuongoza na ku-manage magari hapa mjini wakati utatuzi wa gharama zaidi ukifanyiwa kazi. ni mara nyingi sana tuko barabarani, upande mmoja ukisubiri kuruhusiwa hata kwa nusu saa bila sababu yeyote.

Hapo bado hatujazungumzia matatizo ya umeme ambayo huleta mzozo mkubwa sana kwenye traffic lights pale ambapo umeme hukatika. Na pia kwa upande mwingine, sheria SI msumeno hapa kwetu. nimekuwa nikipigiwa honi mara nyingi tu kwa sababu nimesimama kwenye taa nyekundu wakati hakuna magari. sasa najiuliza, tunasimama kwa kufuata taa au kwa kuangalia kama kuna magari ya kutuzuia kuendelea na safari? Vilevile tunao madereva wengine ni waliyoelimika, wazee wenye heshima zao kwa vijana ambao daima wana haraka kuliko watu wengine, taa imewaka nyekundu bado wanalazimisha kuendelea a safari hivyo kuziba makutano makubwa ya barabara na kusababisha msongamano usiyo na msingi. Pia madereva wa daladala na texi wana sheria zao wazijuazo wao wenyewe ambazo husababisha matatizo na maudhi makubwa sana barabarani…si ajabu sheria zingekuwa zinafuatwa, na wakiukwaji kuchukuliwa sheria, matatizo ya misongamano yasingekuwa kama yalivyo.

swala lililotajwa na wachangiaji wachache la Public Transportation au usafiri wa umma ni muhimu sana. Tena ndio laweza kuwa suluhisho pekee la msongamano. mimi binafsi ni mmiliki wa gari ila kungekuwa na usafiri wa umma ambao ni wa kiwango kiridhishacho,kitoshacho, unaojali muda, na unaoniwezesha nifike nyumbani, kazini na mahala pengine ninapohitaji kwenda bila bughudha, ningeuza gari nipande mabasi au treni kama ndio ambazo zingekuwepo. tatizo hapa ni kwamba, mabasi yetu (hiace na coaster) ni yenye usumbufu mkubwa mno, kwanza ukiwa na shati au blauzi nyeupe, ukifika ofisini unaweza ugombane na bosi wako (utaambiwa hukulala nyumbani au umevaa nguo chafu). unapogombania basi na kubanana na mtu mwenye samaki au nyama ndani ya basi livujalo, linalofuka moshi na lenye vumbi, grisi na matope ni wazi lazima ubughudhike. kwa mliobahatika kufika ulaya, au marekani, wamiliki wa magari ni wachache na ni kwa ajili ya matumizi binafsi sana, hapa tunalazimika kununua magari  kwa sababu ya usumbufu tuupatao kwenye mabasi yetu. Pia usafiri wa umma ni wa kiwango cha juu sana, viongozi wa serikali wakiwemo mawaziri na suti zao hupanda treni na mabasi…suluhisho la hili hapa kwetu ni serikali kuwa serious kwenye swala zima la usafiri wa umma hivyo yaweza kuingia ubia na hawa hawa wamiliki wa ma-hiace na ma-coaster na kuwa na mabasi yenye viwango vya kimataifa ambavyo watu wa aina yeyote, mwenye suti au mwenye kandambili, mwenye mbuzi na mwenye laptop watapanda na kuketi kwa amani. mabasi ya namna hii ni ambayo hata tiketi zake hununuliwa kwa mwezi. waweza kuwa na tiketi ya wiki, mwezi, mwaka au miaka, na itakuwezesha kwenda sehemu yeyote ya dar es salaam bila kuanza kubadilishana masimbi(coins) na makondakta ambao baadhi pia ni chanzo cha uchafu. ila hii inahitaji mpango madhubuti na wataalamu kama wahandisi wa usafiri (transportation engineers) na wadau wengine kama wananchi wenyewe, wamiliki wa hayo mabasi (kama si serikali yenyewe) n.k...tukiwa na usafiri wa namna hii, nani atataka kwenda na gari mjini au kupoteza pesa nyingi kwenye petrol wakati tiketi ya sh. 30,000 kwa MWEZI yaweza kukupeleka kokote hapa DSM pasipo kulipia nauli kila upandapo basi lingine?kwa watumiaji wa magari, mafuta ya sh. 30,000 unayatumia kwa muda gani?

 
     

MICHAEL ATHUMANI MPOMBO  : Friday, June 11, 2010    
  Suala la kwenda Dodoma tushaanbiwa kuwa hiyo ni ndoto hivyo, hilo tuliache kwa sababu jibu lake tunalo. Niliposema Dar Mpya siamanishi kuwa na Dar ambayo ni mji kama Morogoro bali ni kwa kupanua jiji la Dar kwa kujenga ofisi, mabenki, maofisi ya mashirika mbali mbali ya kitaifa na kimataifa, ofisi za balozi mbalimbali, mahoteli, kwenye maeneo yaliyo pembezoni mwa Dar ili kupunguza msongamano wa magari na watu. Hii itasaidia kuwagawa watu kuzifuata huduma hizi huduma hizi mahali zilipo na katika mpango huu mpya ni laazima uwe wa makusudi kabisa na usije tena ukaleta tatizo kama lililopo Dar City Centre maana tutarudi palepale. Hii inatakiwa planners wapange na kuforecast for the next 100 years kwa kuzingatia ukuaji wa idadi ya watu na shughuli za kiuchumi  na jamii. Kwa kufanya hivyo wataweza kukabilkiana na dhoruba kama zinavyotukabili hivi sasa. Miundo mbinu katika sehemu hizi iwe ya kuzigatia ukuaji wa idadi ya watu na shughuli za kiuchumi na kijamii kwa miaka 100 ijayo.
 
     

boniphace makene  : Friday, June 11, 2010    
  Michael, kutokana na hoja yako, je suala hapa ni kuwa na Dar mpya au kwenda Dodoma? Nini maana ya Dar mpya ama ni hoja sawa na kujenga mji mpya sawa tu na kuwa na Morogoro kama mji ambao unapangwa kuwa wa mfano unaoweza kuwa na miundombinu na vyanzo vya kiuchumi na kisha usio na msongamano, au tutafute mbinu ya kugawa shughuili za kiuchumi mathalani kujenga mji wa viwanda, mji wa mambo ya kilimo na mji unaohusika na ufugaji?  
     

MICHAEL ATHUMANI MPOMBO  : Thursday, June 10, 2010    
  Kiasili, mahali popote penye mkusanyiko wa watu ujue kuna jambo aidha ni jambo jema au baya. Suala la watu kujazana Dar na wakati inchi yetu ina maeneo makubwa mengi ambayo hayakaliwi na watu na bado ni mazuri tu linatokana na mtizamo wa watu na hali halisi iliyopo mahali husika. Kwa mfano, kwa Dar watu wanakuwa wengi sana kwa sababu fulani fulani ambazo zinaweza kuwa za kijamii au za kiuchumi. Miundo mbinu ilyopo Dar ambayo ni ya kiuchumi na kijamii ndiyo inayowafanya watu kujazana mahali hapa kwani kwenye watu wengi ndiko riziki inakopatikana na shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii ndiko zinakofanyika. Ukiangalia Dar kuna bandari ambako bidhaa nyingi kutokea inchi za inje hupitia, kuna uwanja wa ndege, kuna ofisi za balozi mbalimbali za inchi za inje, kuna maofisi ya serikali (ikiwemo Ikulu, wizara mbali mbalimbali,n.k), kuna ofisi za watu binafsi, mabenki, mashirika ya kitaifa na kimataifa, mahoteli, n.k. na yote haya ukiangalia kimuundo yako mahali pamoja na kila mtu anahitaji huduma kutoka kwenye ofisi hizi. Hivyo, kwa sababu hiyo ni laazima watu wote watalazimika kwenda mahali pamoja ili kupata huduma hizi tofauti na ukilinganisha kama huduma hizi zingekuwa zimesambazwa katika maeneo mbalimbali ya Dar. Hivyo ni dhahiri kuwa suala la kimuundo ndilo linalofanya kuwa na msongamano wa watu na magari kwaajili ya kupata huduma hizi. 
Michael.    
 
     

MICHAEL ATHUMANI MPOMBO  : Thursday, June 10, 2010    
  Kutokana na mawazo mbalimbali yaliyotolewa na wachangiaji mbalimbali wa mada hii, inaonekana dhahiri kuwa wazo la kuwa na Dar es Salaam mpya ni wazo zuri ingawa lahitaji kuwa na rasilimali ili kulitekeleza. Sisi kama wachangiaji na wadau wa wa jambo hili tukifikiri kwa umakini, je kuna utayari wowote wa viongozi wetu wa serikali kuu na serikali za mitaa ya Dar es Salaam kulifanyia kazi jambo hili kwa kuzingatia mawazo yetu tuyatoayo kwenye mjadala huu?Kama hakuna utayari wa kulishughulikia jambo hili, tujiulize hii inasababishwa na nini na sisi kama wadau tufanye nini kuhakikisha serikali na viongozi wake wanasikiliza mawazo yetu ili kutatua shida ya msongamano wa magari katika jiji letu la Dar es Saalaam?

Ninaamini, kama serikali ingelikuwa na utayari wa kuhamia mji mkuu wetu wa Dodoma, shida ya msongamano wa magari ingekuwa ni ndogo sana!Lakini kwa sababu suala hili tumeambiwa kuwa limebaki kama ndoto tu na halitakuja kutekelezeka katika nayakati za usoni, tutafute njia mbadala kama hizi za kuziondoa ofisi mabalimabali za serikali, huduma zingine za kiuchumi na kijamii kwa kuziondoa katikati ya jiji na kizipeleka inje ya mji ili kuondoa msongamanio wa magari uliopo. Katiak jambo lolote ni lazima kuwe na majaribio, kwa mfano tunaweza kuhamisha ofisi moja kubwa na kuiweka inje ya mji kuona mabadiliko chanya yoyote ambayo yatatokana na utekelezaji huo. Baada ya hapo tutakuwa na uhakika kuwa tunachofanya kitasaidia kuliondoa tatizo au kulipunguza kwa kiwango fulani.

Ni wasaa wa kuchukua hatua kwa kuwashinikiza viongozi wetu kulivalia njuga suala hili kwa lina madhara makubwa kijamii na kiuchumi kwa taifa letu. Hata tunaposema kuwa tunatengeneza mazingira bora ya uwekezaji, kwa Dar es Salaam tunapata wawekezaji wachache kutokakana na miundombinu yetu kuwa mibovu hasa tukizingatia suala la muda katika maendeleo ya mwanadamu na taifa lolote ni la kuzingatiwa na mtu anapopoteza masaa matatu barabarani bila kuzalisha ni hasara kwa serikali na taifa letu kwa ujumla. 
Hivi kweli Taifa hili limekosa viongozi ambao wana uchungu na maendeleo ya taifa lao na watu wa taifa hili? Hivi kweli maendeleo yanapatika kwa kujilimbikizia mali na kusahau kuweka miundombinu ambayo ingekufaidisha wewe kama kiongozi kwa sasa na taifa letu na kizazi kijacho?Tumeingiliwa na mdudu gani huu ambaye ni mbaya kuliko hata virusi vya ukimwi!Ni suala la mtizamo unaosababishwa na choyo zetu na uchu wa madaraka na mali ambazo hata hivyo mwisho wa siku tutakufa na kuziacha hapahapa!Kwa nini tumekuwa wabinafsi mno?Tunasahau collective responsibility tuliyo nayo kwa watanzania maana ndo waliotupa kura ili tuwatumikie na mwisho wa siku hii ndiyo feedback tunayowapa! Sisi kama wadau wa suala hili lazima tuwe na mkakati wa makusudi wa kuendelea kuwaelimisha watanzania wennzetu juu ya nini kifanyike kupata uongozi bora ambao utajali maslahi ya watanzania wote kwa ujumla!Kila siku tunapiga kelele, lakini kelele hizi ni za wachache ambao kidogo tumepewa maono, watanzania walio wengi na ambao hawawezi kuchambua na kutambua kwa nini leo hii wao wanaishi  maisha haya wanahitaji kuelimishwa ili wafahamu ukweli huu na waufanyie maamuzi. 

Tukiwa katika mjadala huu, suala lililopo hapa na linalosabisha msongamano wa magari Dar es Salaam ni suala la kutokuwa na uongozi bora na unaojali maslahi ya watanzania kwa hivi sasa na baadae.

Shukrani, 
Mpombo Michael.           
 
     

boniphace makene  : Thursday, June 10, 2010    
  Bdo naamini kila mwananchi wa Dar es Salaam ana nafasi yake katika kuopunguza ama kuongeza msongamano. Si kweli kuwa maisha bora katika Tanzania yako hapa Dar, lakini kwa nini watu tunakimbilia hapa na kujazana hapa wakati nchi ni kubwa na ina maeneo mengi mazuri tu. Je, hoja ya watu kujazana hapa hata wasio na kazi ni kweli inachangia msongamano, na kwa nini tunajazana Dar na si kwingineko  
     

boniphace makene  : Thursday, June 10, 2010    
  Bdo naamini kila mwananchi wa Dar es Salaam ana nafasi yake katika kuopunguza ama kuongeza msongamano. Si kweli kuwa maisha bora katika Tanzania yako hapa Dar, lakini kwa nini watu tunakimbilia hapa na kujazana hapa wakati nchi ni kubwa na ina maeneo mengi mazuri tu. Je, hoja ya watu kujazana hapa hata wasio na kazi ni kweli inachangia msongamano, na kwa nini tunajazana Dar na si kwingineko  
     

Omari Mwinyi Khamis  : Tuesday, June 8, 2010    
 

Angawaje ni kweli homa ya uchaguzi inafanya viongozi wa siasa wawe katika harakati za kuchaguliwa.Lakini wanaotekeleza ujenzi wa Dar es Salaam si Rais wala Wabunge wetu bali ni manispaa ya Dar es Salaam.Watu hawa ambao ni wafanyikazi wa manispaa ya Dar es Salaam wengi wao wameajriwa mpaka wakati ambao wenyewe watastaafu isipokukwa tu ni Mayor ambaye anachaguliwa kwa muda maalum.Kwa hiyo Demokrasia hapa sio kikwazo ambacho kinazuia ujenzi wa Dar es Salaam mpya.Mbona Dodoma imejengwa wakati wa Demokrasia?Haina haja ya kuongeza wakati wa Rais kwa vile yeye hashughuliki na mambo ya ujenzi wowote isipokuwa ni uongozaji wa nchi nzima na utulivu wa nchi.

Kwa ufupi ndugu Novatus anaona kwamba kwa kiswahili twasema SUBIRA HUVUTA KHERI. Ni kwamba tukisubiri hata hiyo Dar es Salaam mpya (kama daraja la mto wa Rufiji) pia itajengwa.Pia sisi waswahili tunao msemo wetu BANDU BANDU HUMALIZA GOGO.

Linalohitajika sasa ni hao watu wa manispaa ya Dar es Salaam wawe na mpangango wa miaka kumi(2010-2020) ya kuujenga mji mpya wa Dar es Salaam.Wangeweza kuichukuwa ile PLAN ya jiji la Dodoma na kufanya marekebisho kuhusu barabara ziwe pana na ziwe na nafasi ya magari manne kila upande mmoja.Wataalamu wale wale ambao walihusika na ujenzi wa Dodoma wapewe nafasi ya uejenzi wa Dar es Salaam mpya:Wengi wao bado wapo nchini.


Dr.Khamis

Sweden

 
     

Novatus  : Tuesday, June 8, 2010    
  Mipango ya muda mrefu na inayotekelezeka ni kitu cha msingi. Dar inahitaji wataalam wa miundo mbinu waiandalie mipango ya muda murefu na utekelezaji uanze kidogokidogo. tunaweza kuona mifano michache kwa vitu vilivyokuwa ndoto lakini vikatekelezeka. Daraja la mto Rufiji ilikuwa ni ndoto ya siku nyingi lakini kwa mikakati na umakini wa uongozi husika lilijengwa. Uwanja wa taifa ambao ukiwa ndani yake nivigumu kuamini kama upo Temeke umejengwa na hata Nchi kama Brazil wachawi wa soka duniani wamekuja na kucheza hapo.Barabara nyingi mpya za rami toka mkoa hadi mkoa zimejengwa, kwa mifano michache hiyo naamini kila kitu kinawezekana ingawa vingine vinaweza kuchukua muda. Hivyo nia,dira,mikakati,ubunifu na uzalendo vinaweza kutufikisha popote tunapotaka. Rasilimali zipo changamoto ni kuzitambua na kuzitumia.  
     

S. Moyo  : Tuesday, June 8, 2010    
 

Habari Makene


Mchango wako umeanika mambo makuu mawili ambayo nadhani ni vyema kuyafikiria kwa umakini. Kwanza unaweka wazi kuwa uchaguzi umekuwa kikwazo cha Dare s salaam mpya. La pili ni bei ya mafuta ni kubwa zaidi ya nchi kama marekani na afrika kusini yenye magari mengi zaidi ya DSM.


Ukweli ni kwamba democrasia ya uchaguzi inazitesa sana inchi za Africa. Kwa miaka yote mitano  ni kwamba viongozi wetu wanajikuta katikati ya sintojua kati ya kutekeleza program za maendeleo au kuwekeza katika vivutio vya wapiga kura visivyo na tija kwa maendeleo. Hii ndio maana mipango endelevu haiwezekani hata kidogo. Kwa mawazo yangu katika miaka mitano ya uongozi Rais kwanza anamwaka mmoja wa kulipa madeni ya uchaguzi. Madeni haya mengi ni yale aliyosaidiwa na watu binafsi. Mwaka huu wa kwanza anautumia pia  kuweka viongozi madarakani na kutengeneza serikari. Hivyo hakuna la maana linaloendelea juu ya maendeleo ya kweli. Mwaka wa pili anautimia kutafuta pesa ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuomba misaada toka kwa wahisani. Mwaka wa tatu ndo anafanya kazi kiasi. Mwaka wanne anaanza kujikusanya kutafuta wahisani na wafuasi ili achaguliwe mwaka unaofuata. Hii ni pamoja na kupambana na wapinzani wake ndani ya chama chake na nje. Kumbuka juhudi za kutengeneza kamati za uchaguzi kwa ajili ya mgombea wa CCM ilianza mwaka jana. Mwaka huu ndo mipango imekamilika ndo ukusanyaji pesa unaanza. Hii ni kutokana na mafanikio ya mipango iliyoanza mwaka jana. Maana yake nini> Ni kwamba tangia mwaka jana kipaumbele ni mipango ya uchaguzi. Mambo mengine YA MAENDELEO YALISIMAMA tangia hiyo 2009. Mwaka huu ndo usiseme. Hata wabunge wanazungumzia majimbo na sio EPA wala RICHMOND wala barabara za DSM. Watuhumiwa wa ufisadi ndo kwanza wanapumua na wenyewe wapo majimboni kwenye kampeni. TUNAISHA KWA KUKOSA MAARIFA. Na wala TUSITAFUTE MCHAWI. KWA KUIGA DEMOKRASIA YA MAGHARIBI HATUTAFIKA. Ukifuatilia analysis yangu utagundua Rais anamwaka mmoja tu kutekeleza MIPANGO HALISI YA maendeleo ya kweli bila kusukumwa na PRESSURE YA siasa NA UCHAGUZI.


Inatakiwa wote tukubali kuwa si rahisi kila mtu kuwa RAIS. Inatakiwa KUWAPO MUDA WA UTULIVU AMBAO KIONGOZI HATAKUWA NA MISUKUMO NA UTATANISHI WA UCHAGUZI juu ya kukilinda kiti cha urais au siasa. Uwe ni muda wa Rais kufanya kazi za maendeleo kwa miaka kadhaa kabla ya uchaguzi kusogea. Na hii itawezekana ikiwa rais atapewa muda mrefu kwa rais kufanya kazi. Yaani muda wa kutosheleza angalau kumalizia jambo moja. Mfano Daraja la mkapa limeanza awamu ya mkapa limeisha wakati wa kikwete. Je nani atapenda aanzishe jambo litakalomaliziwa na mwimingine. Ukifikiria kijuu juu na kusahau ubinadamu wetu utasema hili halina maana, lakini binaadamu ndo walivyo. Hata wewe uko hivyo. HIVYO TUJARIBU AWAMU ZA MIAKA NANE NANE MADARAKANI ILI KUMPA RAISI MIAKA MINNE MPAKA MITANO YA KUTEKEREZA MIPANGO YA MAENDELEO NA MIAKA MITATU YA KUJIWEKA SAWA KWA UCHAGUZI. Nadhani  RWANDA INAFANYA HIVYO. UTULIVU UTAPATIKANA NA MIPANGO YA MAENDELEO ITAWEZEKANA.


Inaendelea hapo chini

 
     

S. Moyo  : Tuesday, June 8, 2010    
 

Imeanzia hapo juu

Jibu ni moja tu, sisi sote tuzungumzie kubadiri mfumo wa uongozi. Na hii sio kubadiri chama. Kwenye mfumo uliopo kujiingiza kwenye miradi mikubwa itakayotekelezeka kwa machungu itakuwa ngumu. Tuache kufikiria kuwa kunakiongozi atakae kuwa na akili na uwezo kuliko mwingine. Kinacholeta maendeleo ni mfumo na sio mtu. Mfano Rais wetu awekeze kwenye kujenga barabara za DSM, je watu wa huko madongo poromoka atawafikia lini, mishahara ya wafanyakazi aiweke sawa lini, na nilini atakapogundua kuwa BUSHI alidanganya juu ya pesa ya barabara. Mgabe kakaa kwa muda mrefu sana madarakani ndio maana anaujua kila ulaghai wa democrasia ya Magharibi. Ndo maana wazungu wanamtaka mtu mwingine wakumdandanya ili baada ya miaka mitano aondoke na kuja mwingine. Mimi siwalaumu viongozi, nalia na mfumo. WAZUNGU WANAKILA PESA WANAYOIHITAJI NDO MAANA HATA WAKIKAA MWAKA MMOJA MADARAKANI KWAO MIPANGO ITAENDA TU. Kwa sisi kilomita tano tu za barabara ya lami inahitaji ufadhili, na paper work ili upate pesa ya mfadhilki itachukua miaka mitatu mpaka mitano. Ukipeleka request leo, mtekelezaji yawezekan ikawa Rais wa tatu baada ya wewe. (Ulizia mtwara korido plani utajua ni lini mipango ilianza na mpaka sasa iko wapi na itatekelezwa lini. Au je vitambulisho vya utaifa, viliaza linini kuzungumziwa, na leo tuko wapi. Tenda tu imechukuwa miaka zaidi ya mitano na mabunge kadhaa yamezungumzia hilo).


Tusahau maendeleo mpaka mipango yetu wenyewe itakapo wekwa sawa. Tutaishia kulaumiana wala suluhisho halitakuwepo.


Tuwaachie wenye akili wale (wazungu). Wakishiba watatupangia mipango wa kusafisha meza (climate change) na namna ya kutunza mabaki ya vyakula walivyo dondosha wakiwa mezani (used car and dumping grounds for poisonous materials).


Moyo  


 


 
     

Omari Mwinyi Khamis  : Monday, June 7, 2010    
 

Ndugu zangu kwanza sio kweli kwamba wanaomiliki magari Tanzania ni matajiri kuliko wale amabo wanamiliki magari Tokyo, London au Amerika.Bei ya mafuta ya petroli huwekwa na serikali ya nchi.Kwa hiyo huenda Serikali ya Tanzania imepandisha kodi ya mafuta hayo.Pia umbali wa kusafirisha mafuta hayo inagharimu fedha nyingi.Kwa hiyo kuna sababu kadhaa ambazo zinafanya bei ya mafuta kuwa uko juu huko Tanzania.Wenye vituo ya petroli pia wanataka faida.Mafuta yanauzwa katika dolla na dolla ukiwa kubwa sana kulingana na shililingi zetu za Tanzania inasababisha bei kupanda na hivi karibuni Dolla moja ilikuwa ni kiasi cha 1400 Tsh.

Kama waziri ana msimamo huo kwamba kuhamia Dodoma ni kama ndoto basi kwa nini serikali ilisisitiza kujenga mji wa Dodoma kama mji mkuu (Capital)?Kwa nini fedha nyingi zilitumika kwa ajili ya ujenzi wa Diodoma toka mwaka 1975  mpaka sasa hivi ikiwa msimamo wa serikali ndio huo ambao unatolewa na waziri? Kwa nini tusijenge Dar es Salaam mpya toka 1975 kwa vile tulikuwa na ufununu kwamba hapo mbele(baada ya miaka 10 au 30) tutapata matatizo ya usafiri Dar es Salaam? Tumepoteza wakati wetu bure kuishughulikia Dodoma na sasa tunalipa malipo ya uzembe wetu.

Sisi Waswahili wa pwani twanena AKILI NI NYWELE KILA MTU ANAZO!

Dr.Khamis


Sweden

 
     

boniphace makene  : Tuesday, June 1, 2010    
  Ndugu Kachwa nafurahia mchangio wako. Ni kweli hatuna magari mengi kama Joberg, Tokyo ama London. Lakini huko kote bei za mafuta ziko chini ukilinganisha na hapa. Inawezekana pia kuwa wamiliki wa magari hapa ni tajiri sana ndio maana bei ya lita moja hapa ni bei ya lita nne kwa Marekani.

Ni wazi pendekezo la Dar es Salaam mpya halikuzingatiwa katika bajeti ya mwaka huu na jambo hili lina sababu nyingi; mosi huu ni mwaka wa uchaguzi hivyo tunatakiwa kudunduliza fedha kwa ajili ya kazi hiyo, pia uchumi wa dunia umehitilafika sana mwaka huu na sisi ni sehemu ya dunia hiyo na tatu, wafadhili wamepunguza misaada yao katika bajeti. Nimemsikia waziri mmoja akizungumza kuwa kuhamia Dodoma ni ndoto, atakayekumbuka hili anisaidie maana nadhani limeandikwa magazeti ya leo. Je, kama hali ni hii na kwa utajiri huu wa wana Dar es Salaam wanaouonyesha katika kununua mafuta kwa nini tusiwe na mchango maalum kwa ajili ya kutanua barabara zetu?
 
     

Omari Mwinyi Khamis  : Tuesday, June 1, 2010    
 

Thanks Mr. Kachwa.Well we have failed to move government ministries to Dodoma-Capital.Since 1975 to date only The Prime Minister’s Office has moved to Dodoma. It was supposed also foreign embassies should move to Dodoma but that is not the case. We can build flyovers, use trains (trams) for transportation but there is no space for such things in the 2010/2011 budget.

The building of a New Dar es Salaam is the only way out and will be cost effective.

Dr.Khamis

Sweden

 
     

Rah Kachwa  : Monday, May 31, 2010    
  Hivi ni kweli kwamba Dar tuna magari mengi kama Tokyo, Johannesburg, London etc. kwani viongozi wetu hawaoni miundombinu kwa wezetu wanapotembelea maeneo hayo kikazi. Nimeambiwa mji wa Johannesburg pekee una magari zaidi ya laki tano (500,000) wakati Dar magari yanakadiriwa kuwa 120,000... lkn foleni ya dar ni kubwa maradufu au mara tatu  ya Joh'burg..  
     

Rah Kachwa  : Monday, May 31, 2010    
  Sharti la kuwa diwani au mbunge ni kujua kusoma na kuandika, regardless umesoma mpaka wapi na una uzoefu gani wa kuongoza.

Naomba wazawa tujitokeze kwa wingi mwezi octoba 2010 na kuwachagua viongozi watakaotufaa kwa miaka mitano ijaayo. Pia wenye uwezo wa kuwa viongozi wachukue fomu za maombi na waigie kny mchakato
 
     

Rah Kachwa  : Monday, May 31, 2010    
 

LGAs ziwezeshwe in terms of human capital ili ziweze kutimiza malengo. Pia katika uchaguzi ujao madiwani wasio na sifa wasichaguliwe. Kumbuka hawa madiwani ndi wanakuwa kny bunge la wilaya almaaruf kama 'FULL COUNCIL'. kwa hiyo tusidhaarau kura zetu oct 2010. Pia wenye uwezo wagombee

 
     

Rah Kachwa  : Monday, May 31, 2010    
  Inakuwaje unamkabidhi mhasibu asiye na sifa mabilioni ya fedha ya maendelo ya wananchi na kumwacha mwenye sifa (mf CPA)?? je ni busara hii??  
     

Rah Kachwa  : Monday, May 31, 2010    
  Kwa mfano mpaka sasa halmashauri ya wilaya yangu Bukoba vijijini haina mhazini (District Treasurer). Aliyekuwpo amestaafu. Hivi ni kwamba TAMISEMI haioni hili tatizo la ukosefu wa proffessional staff na kuona umuhimu wa kuajiri na kutoa maslahi mazuri kama retention policy. Kwa sheria na kanuni za serikali za mitaa (LGAs) ili mhasibu athibitishwa kuwa mkuu wa idara inabidi afanye kazi kwa miaka isiyopungua saba (7). Na hii inapelekea idara nyingi kuongozwa na watu wasio na sifa ambao wameweza kuvumilia kwa miaka saba. Hivi TAMISEMI haioni kuwa hiki kipengele kimepitwa na wakati????


Ndimi,
Rahim Mzee Kachwamba (Dsm, Tz)
 
     

Rah Kachwa  : Monday, May 31, 2010    
  Mpango wa kupeleka huduma karibu na wananchi kny halmashauri zao (Decentalisation by Devolution) utafanikiwa tu endapo utahusisha pia human capital reforms. Kuendelea na watumishi wa umma wasi na ujuzi wala uelewa wa masuala nyeti ni kupoteza pesa ya mlipa kodi (mismanagemnt/misallocation of public funds)..

Rgds,
Rahim Mzee Kachwamba
 
     

Rah Kachwa  : Monday, May 31, 2010    
 

All Feeder roads should be macadamised (tarmac)... ie barabara za mitaani ziwekwe lami.
Hoja ya rafiki yangu Boniface Makene ina mashiko (valid). Kuziacha barabara mikononi mwa halmashauri zenye tuhuma za ubadhirifu wa fedha za umma ni kuwanyima wananchi haki ya huduma nzuri ya barabara. Anyway Im told kwamba siku hizi kuna 'Watanganyika' na 'Wadanganyika', pia 'Wananchi na Wenye nchi' .... Tofauti ya utajiri kati ya walio nnacho na wasio nacho inazidi kuwa kubwa mno. Nashangaa tunajivunia amani tele wakati maeneo kama Mbezi Beach bajeti ya ujenzi wa geti na fence ni kama robo (1/4) ya gharama za ujenzi... Tunajifungia na magrill na siju moto ukitokea ndani tunatokaje maana mpaka ufungue mageti matatu au manne moto ukiwaka ndani ni ngumu.

Rgds,
Rahim Mzee kachwamba (Dsm, Tz) 

 
     

Rah Kachwa  : Monday, May 31, 2010    
  also all Government's Ministries, Independent Departments and Agents (MDAs) should be re-located to the capital city DODOMA and leave Dar for business people. Even H.E. President Jakaya Kikwete should relocate to the capital city DODOMA. Anyway you politicians why don't you leave Dar for business and go to the capital city DODOMA. Why are you not shame of staying in Dar while a hard earned Tanzanians billions have been spent on CAPITAL CITY DEVELOPMENT (CDA) DODOMA...  
     

Rah Kachwa  : Monday, May 31, 2010    
  Complement to the flyers etc, we need to build 'new dars' in the peripheries like Mbagala, Kongowe, Boko, Mkuranga, Kigamboni, Mbezi Kimara, Kibaha, Mbezi beach etc. the famous godowns by the name MLIMANI CITY is a vivid example on how new dar could decentralise the dar central business city...  
     

Rah Kachwa  : Monday, May 31, 2010    
 

From the process improvement theories and postulates, it is believed that to improve an overall slow process where the process has got some bottleneck stages (slow), you need to catalyse the process at bottlenecks so that it becomes faster and at the same improving the speed of the whole process.
therefore for Dar es salaam roads the bottleneck stages are kny mataa
(lamp robots) and therefore building flyers, side roads or undeground roads could improve the whole road movements, and we could get rid of these queues in Dsm

By Rahim Mzee KACHWAMBA (dar, tz)

 
     

Omari Mwinyi Khamis  : Sunday, May 30, 2010    
 

Ninavyofahamu mimi ni kwamba manispaa kama ile ya Dar es Salaam inayo uwezo wa kuomba misaada kwa serikali kuu na pia nje ya inchi ili kuborosha mji mkuu.Njia zetu za mitaa kuwa na mashimo makubwa na kuweka vidimbwi wakati wa masika ni jambo la kawaida. Na kama njia hizi zinamsubiri Masiha(Nabii Isa) ashuke basi zitasubiri sana kwani ajika hakuna mtu ambaye atafahamu kurejea kwake.Ataishi kama mtu wa kawaida.

Hapo awali tulizungumzia usafiri wa reli kutumia trams ili kusaidia katika ufumbuzi wa msongamano wa magari.Sasa hivi inaonekana serikali in deni kubwa la kulipa hiyo kampuni ya Kihindi (Rites} sh 177 billion wakati Rites haikuboresha reli yoyote na gari moshi lolote na hawakutumia fedha zao hata chembe.Bali walichukuwa TRL kama chambo cha kupatia mkopo.

Kwa hiyo hapa kunanuka rushwa.Rites imepitishwa mlango wa uwani na ikapata mkataba wa reli.Ingawaje tumeahidiwa kwamba infrastructure ni moja wapo ya priority ya serkali sidhani kwamba msongamo wa magari Dar es Salaam utaondoka kwa muda wa miaka mitano inayofuatia!Serikali yetu ina matatizo ya kifehda.

Dr.Khamis

Sweden

 
     

boniphace makene  : Sunday, May 30, 2010    
 

Ndugu zangu;

Jambo la kutazama pia ni kuwa, barabara nyingi zinazounganisha mitaa na vitongoji ziliwahi walau kuona utamu wa lami nyakati hizo kama si za ukoloni ama zile za awamu ya kwanza. Kwa sasa barabara nyingi kati ya hizo zinamsubiri labda Masiha ajitokeze ndio zione lami inawekwa, lakini jambo la kutafakari hapa ni moja?

Nini mchango wa manispaa zetu katika kukabiliana na tatizo la kuwa na barabara mbovu zisizopitika kati ya mta na mtaa?

Je, kuna maingiliano ya wazi juu ya mipango ya kukabiliana na tatizo hili kati ya Manispaa na serikali kuu?

Tujadili

 
     

Omari Mwinyi Khamis  : Thursday, May 27, 2010    
 

Mtu masikini pia naye anataka kitu cha kumburudisha kama gari ndio kile kitu atakacho basi atajihini vitu vingine na kuhifadhi fedha kidogo kidogo mpaka apate kununua gari.

Washwahili tunasema ”BANDU BANDU HUMALIZA GOGO”.Pengine hao ambao wanahusika katika ujenzi wa barabara za Dar es Salaam na vitongoji vyake wanatumia msemo huo wa Kiswahili.

Kweli gari ni nyingi Dar es Salaam lakini sio sababu ilifonya msongamano ukawa kama ugonjwa usiotibika.Manispar ya Dar es Salaam ndiyo ambayo haikuwa na mipango mizuri kwani mia kumi uliyopita waliambiwa kuhusu tatizo hili na walipuuza.Sasa tatizo limetokea wanatapatapa kama kuku mwenye kideri na badala ya kutatuwa tazizo wanavuruga zaidi.

Miji yote mikubwa duniani ina magari mengi.Nilikuwa USA na Canada miaka kama mitatu iliyopita niliendesha gari kati ya Montreal Canada na Washington DC.Wakati nilipofikia nje ya New York City ilikuwa ni wakati wa watu kutoka kaznini na kuendelea majumbani mwao.Lakini hakukuwa na shida yoyote kwa vile kila upande wa barabara kulikuwa na lanes kama sita hivi.Magari yalikuwa ni mengi mno lakini Traffic Lights na waendeshaji wenyewe makini msururwa wa magari ilikuwa ukitiririka kama maji katika sehemu zote mbili.

Wingi wa magari pia ni maendeleo ya kisasa.Katika nchi za Scandinavia kila familia ina wastani wa gari tatu.Idadi hii inahisabiwa kama ni maendeleo.

Sisi watanzania tuna busara sana lakini matatizo yetu mengi yametokea wakati rushwa ilipopamba sana nchini.Hata ticketi ya basi huipati bila kutokwa rushwa na liseni ya kuendesha gari ndio kabisa hiyo rushwa imepamba mizizi.

 

Dr.Khamis

Sweden

 
     

Torokoko, Mzee  : Thursday, May 27, 2010    
 

Thanks ila kwa hili sualla la msongamano wa magari kwa sasa limekuwa kero sana kwa hapa nchini kwetu Tanzania kwa sababu zifuatazo:-


Kwanza kutokana na hali halisi ya miundombinu mibovu iliyopo nchini hapa Tanzania tukiangalia suala la barabara siyo nzuri sehemu nyingi tu hii inatokana na  hali ya maendeleo ambayo hailingani na vyombo vya usafiri vinavyoingizwa hapa nchini hasa magari yanaingizwa huwa ni mengi sana.


vilevile tukiangalia kwa upande mwingine sisi watanzania tunachangia hili kwa kiasi kikubwa sana, utakuta mtu anaishi kenye nyumba ya kupanga, huku anafanya kazi labda kweye kampuni fulani akipata mshahara wake anafikiria kununua magari tu  mala benzi, range rover na hajui kwamba hayo magari atayapaki wapi...? hii inadhihirisha kwamba watanzania wengi tupo kistarehe zaidi na siyo kimaendeleo, ambayo mwishoni inapelekea kuwa na msongamano wa magari barabarani.

Napenda kuwashauri watanzania wenzangu kwamba tuwe na maamuzi ya busara ya kuleta maendeleo na siyo starehe. 
 
     

Omari Mwinyi Khamis  : Tuesday, May 25, 2010    
 

Ngugu Makene kama liseni za barabara ni feki basi matatizo yetu yamekidhiri mipaka.Hili ni swali la wale wanaokusanya kodi kwamba wawe washupavu na wawe wajanja kuliko hao walarushwa.

Kama sikosei ni kwamba fedha nyingi za kujenga mji mpya wa Dodoma (Capital) zilitoka katika nchi kadaa za nje.Itabidi tena kutafuta misaada ili kujenga mji mpya wa Dar es Salaam.Hata tukijenga ”fly overs” si fedha za kodi yetu ambazo zitatumika katika ujenzi wa barabara hizi.

Kwa mfano njia kutoka mpaka wa Tanzania na Kenya/Lungalunga mpaka Tanga itajengwa kwa msaada kutoka USA. Jia hii toka 1961 ilitolewa ahadi ya kujengwa na viongozi wengi.Lakini sasa itajengwa kwa kisasa na haikusababisha ”bomowa ,bomowa” nyingi.

Kitu kingine ni kwamba kama Tanzania tungelikuwa tunaendesha na kumili asilimia hamsini tu za migodi yetu yote ya dhahabu iliyoko nchini, matatizo ya fedha yangelikiwa hayapo.Tanzania isingelikuwa na shida ya fedha hata kidogo.Sasa hivi ounce moja ya dhahabu yauzwa kwa bei ya 1224$ na Tanzania inapata 3% tu ya fedha hizi na kampuni za migodi zinapata 97%.Fedha hizo zote (97%) zinapelekwa nje ya nchi na makampuni hayo.Je mwenye makosa ni nani?

Fedha zetu zajenga miji mingine Ulaya wakati sisi tunasongamana na pia kuwa masikini wa kuomba omba.

Dr.Khamis

Sweden


 


 


 

 
     

boniphace makene  : Monday, May 24, 2010    
  Ni kweli kabisa Dk Hamis, lakini jambo ninalotazama hapa ni moja, ni kweli Watanzania tunaweza kuwa wazuri katika kukubali maumivu na hata kufikia hatua ya kushindwa kutoa suluhisho za matatizo yetu?

Kuna hoja imetolewa na mmoja wa wachangiaji hapa kuwa, hata kama kodi zikiongezwa utatuona tunalipa tu, lakini pia tukumbuke pia upo uwezekano kuwa hata hizi road lisence nyingi ni feki, kwa hiyo inawezekana idara za mapato hazipati fedha inayotakiwa na hivyo kufanya hali kuwa ngumu katika kupata fedha za kutanua miundo mbinu. Kama hili ni kweli, sasa tutapataje fedha za kujenga Dar mpya kama anavyoshauri Dr Khamis?
 
     

Omari Mwinyi Khamis  : Sunday, May 23, 2010    
 

Ndugu Makene sisi watanzania hatuna uhaba wa ardhi sasa kwa nini tusongamane katika eneo la Dar es Salaam ya sasa. Kama nilivyodokeza awali kwamba Dar es Salaam mpya yaweza kujengwa katika eneo kati ya BOKO-Bagamoyo-na Morogoro.Mji huu upya ungelijengwa kwa makini mno ili kuepuka msongamano.Kwa mfano ofisi za serikali zingelisambazwa.Hapa natowa mfano kama wa Amsterdam,Holland kila sehemu ina maduka,hoteli, hospitali,kituo cha polisi na vituo vya mabasi.Kila njia ina sehemu sita,sehemu nne za mgari(kila upande sehemu mbili) na shemu moja ni kwa watu wa baiskeli na sehemu moja ya watu wa mikuu.Mji uwe na vitongogi kama hivi vingi.Amsterdam hakuna daladala bali mabasi makubwa ya abiria tu na ”trams”.

Tumeweza kujenga Dodoma mpya (Capital) lakini tumeshindwa kuhamisha serikali yetu kwenda Dodoma.Ni ofisi ya Waziri Mkuu tu ndio iko Dodoma na Bunge.Hii ni sababu moja ya msongamano wa magari hapa Dar es Salaam.pia idadi ya wakazi wa Dar es Salaam imeongezeka.

 Ndugu Makene ukiwa na nafasi tembelea Amsterdam utajionea mwenyewe jinsi mji ulivyojengwa.Embassy yetu iko Den Haag!

Dr.Khamis

Sweden

 
     

boniphace makene  : Saturday, May 22, 2010    
  Ndugu zangu wana mjadala, nakubaliana nanyi katika hoja nyingi na hasa hii ya kujenga Dar es Salaam mpya, je, wapi Dar es Salaam hiyo ijengwe na iwe na viashiria vipi ili kuifanya Old Dar es Salaam kubakia mji wa kukumbuka kero na hiyo mpya kuwa mithili ya Pradise?  
     

Festo E. Maro  : Thursday, May 20, 2010    
 

Mr. Boniface that options of encouraging companies to buy buses for their employees is short-term solution. On the other I accept there will be traffic reduction in certain hours of the day or week. You should also think that some of these employees have wives and relatives who probably are not employed and know driving. Definitely they will have access to drive those cars for other household transport needs.

Will the buses offer services during week ends and here we have not complicated the situation by considering worker's annual leaves. I think you will appreciate there are more complications than just traffic during office hours.

You should also bear in mind that 90% of economic activities are in the hands of informal sector. You shouldn’t under estimate purchasing power of these folks. Others have unregistered businesses which use vehicles in either distribution of their products or irregular trips to collect debts, send/receive invoices etc... How can these be controlled?

The only viable option is to construct satellite cities and expand existing roads. Fly over’s should be built in road junctions which have high vehicle density.

 
     

Omari Mwinyi Khamis  : Thursday, May 20, 2010    
 

The idea of the employer collecting employees presented by Mr.Makene is familiar to me since STAMICO used this method for its employees in Dodoma as well as Dar es Salaam Office.However, we should not use minibuses since these will cause traffic jams at present time as we have many motorists in Dar es Salaam.

1.The construction of a “New Dar es Salaam” is also a good idea but that city should be built outside the prensent Dar es Salaam and retain the old Dar es Salaam for preserving our history.Most of the modern world citities have preserved their core old cities.

We have always to think in terms of 50 years ahead of us and not just to have a quick solution at present and start again solving the same problem after just 10 years.

Dr.Khamis

Sweden

 
     

Omari Mwinyi Khamis  : Thursday, May 20, 2010    
 

Ndugu Abdallah mawazo ya Eng.Charles Z. Wihenge ni mawazo mazuru mno na sijui  kwa nini wale ambao wanahusuka na matengenezo ya mji wa Dar es Salaam hawakuyafuatilia.Hapa huenda kuna ile kasumba ya kwamba Eng.Charles ni mzalendo kwa vile hawakujali.Kasumba kama hiyo ilinipata mimi wakati nilipojitolea kwa serikali ili kuchunguza migodi ya dhahabu bure bila kutaka mshahara wowote.Walipuuza na halafu wakaajiri kampuni ambayo baadaye wakalipa fedha nyingi za bure na ikaleta mgogoro.

1.Kweli zamani hatukuwa na msongamano kwa vile usafiri wa abiria wa jijini ulikuwa ukifanywa na KAMATA kwa kutumia mabasi makubwa.Sasa hivi tunatumia hata pikipiki ndogo na mabasi madogo ambayo yanasabisha msongamano.

2 Kuhusu usafiri wa train kama” Trams” pia ungelisaidia usafiri mfano huu unatoka katika miji mikubwa kama Paris au Amsterdam.Mji kama Amsterdam hauwezi kutumia ”underground trains” kwa vile nchi yenyewe iku chini ya maji(sea water level).

3.Usafiri wa baharini kwa vitongoji  vya Dar es Salaam pia ungelisaidia kupunguza msongamano.

Kifungu cha pili na cha tatu vinahitaji fedha nyingi na sasa serikali haina fedha.Lakini kuhusu mabasi makubwa hawa ambao wana daladala wangeliunda kampuni moja na wakasaidiana ununuszi wa mabasi makubwa.

Dr.Khamis

Sweden

 
     

boniphace makene  : Wednesday, May 19, 2010    
 
Its my pleasure to post my comments in this group mail so that it can be heard by policy makers.
 
If we want to get rid of the traffic woes in Dar es Salaam roads we need to be more creative and innovative, than using excessive resources which could cause more harm to the economy.
 
First Option:
 
The Government should encourage organizations in the private sector which are paying VAT to purchase/import between two to seven minibuses free of charge (No import tax, VAT or any taxes to be levied for the minibuses) so that employees may use the vehicles when coming and going back to work. The employer will agree with employees on the best ways to manage the routes efficiently and effectively as well as operations costs.
 
The best example is the way BoT, Tanzania Road Haulage and Swissport manages its staff minibuses on daily basis. If this is implemented successful, we are sure of removing more than 200,000 vehicles in the road during peak hours.
 
For example:
 
32 Banks each with average of 200 employees in DSM, 75% having vehicles it means
nearly 5000 vehicles will be removed from the road during peak hours.
 
Telecom companies with more than 4,000 staff at DSM only, 80% having vehicles, it means about 3,200 vehicles will be removed from the road during peak hours
 
If the Government ministries and its agencies like (TRA with more than 3000 staff in DSM, TPA with more than 500 staff in Dar) will also do the same, it means that, in no time there will no longer be traffic jams during week days.

NOTE: The traffic jam in DSM is also contributed by many Government vehicles. To prove this point, let's watch the number of vehicles on the road during the budget week when many Government officials are in Dodoma. It hardly take 10 minutes to drive from Mwenge junction to Salander Bridge or even city centre. Thats why i keep on insisting that, the Government should also purchase the minibuses to discourage its staff from using private vehicles.
 
Second Option:
 
If we want to get rid of the traffic jams in the city, we need to construct the so called New Dar Es Salaam. I found this type of construction in Luanda Angola. People are being evacuated in phases, and construction of high rising buildings, four lanes tarmac roads in between the buildings and many other important infrastuctures such as clean water supply and sewarage drainage systems are constructed.

Giving an example, evacuation can be done for the people living in the square between Karume Junction, Buguruni, Tazara and Chang'ombe traffic lights. The Government agency (NHC or Pension funds or joint program) construct about five to ten large high rising structures like the Benjamen Mkapa Tower, which are enough to accomodate all the people in that area.

All the people in that square are given an appartment to stay in those ten buildings. The rest of the area is demolished and high rising structures are built in the remaining area of the square, and accomodate people from another square as well. This evacuation and reconstruction process can go on until the whole city status changes.

The appartments are not given free of charge like NHC ones. People buy them using special policies and guidelines by the agency and the mortgage bank.

Third option - SUMATRA WASIWE WAKWASI

Implementation of "Executive transport system" whereby private companies will be allowed to operate executive bus business which have well planned schedules and which are neat, with air conditions etc. Even though the charge will be TZS 3,000 from Tegeta and Mbezi Beach (or TZS 6,000 return ticket), people will pay the fare so long as they are sure of getting the transport on time and without scrumbling.

Next time i will give more options WHEN I HAVE TIME TO DO SO

Stay blessed
 
     

boniphace makene  : Wednesday, May 19, 2010    
  Ndgu Nyenga na Hamis, nakubaliana nanyi katika baadhi ya hoja hasa suala la kudhibiti magari kuingia mijini. Lakini ili tuweze kuweza kufanikisha jambo kama hilo nadhani tunahitaji kuwa na usafiri wa umma ambao upo wakati wote na wenye viwango? Huko nyuma tulikuwa na Uda lakini ikafa taratibu na sasa imebaki kama mgonjwa anayesubiri siku zake zifike.
Je, taweza kweli kuwa na usafiri wa umma ambao utakuwa imara na safi kwa watumiaji?
Je, kama kodi zinzolipwa na watumiaji magari ni nyingi kama tunavyobainisha, kwa nini tusiwee na kodi maalum ama mchango maalum kwa ajili ya utanuzi wa barabara na mchango huu ukawahusisha wanachi wote waishio jijini hapa?
 
     

nyangubho nyega  : Wednesday, May 19, 2010    
  Mh ndugu yangu hiyo ya kodi ni ngumu sana. upandishaji wa kodi unazingatia mambo mengi na si kuangalia msongamano tu. Lakini pia watanzania wengi pesa iko mikononi mwao kuliko hata serikali. Kodi kila siku zinapanda za vitu mbalimbali, ulishasikia watu wakagoma au kushindwa kulipa? labda wa vijijini! tunalalamika, maisha yanaendelea.  
     

Omari Mwinyi Khamis  : Wednesday, May 19, 2010    
 

Ndugu Makene kodi zikiwa nyingi sana zinaharibu nchi kwani mtu anaponunua gari lake tayari ametoa kodi.Vitu ambavyo vitapunguza magari kuzurura bila ya sababu mjini  ni kuongeza malipo ya parking za magari kwa saa na kuweka ”Camera” nyingi mjini ambazo zitaweza kuhifadhi nambari za kila gari ipitayo njiani ili muendeshaji gari alipe kiasi kadhaa .Mfano nimetowa awali kwa kiwango cha 1000 Tz.sh. kwa kila mara ambapo nambari ya gari inapohifadhiwa kwenya kamera.


Wazo jengine ni kwamba serikali ingejenga mji mwingine nje ya Dar es Salaam na kuuwacha mji wa zamani kama ulivyo ili kuhifadhi historia yake kwa vizazi vijavyo.Mji huu mpya ungelijengwa kwa makini sana ili tuepuke msongomano si wa magari tu bali ya hata ya nyumba.Ofisi za serikali zingelisambazwa na kila eneo lingelikuwa vitu vyote vinavyohitajika katika maisha ya kila siku kwa mfano maduka,hospitali,kituo cha polisi,shule na hoteli.


Dr.Khamis


Sweden

 
     

Festo E. Maro  : Wednesday, May 19, 2010    
 

Wakati unapofikiria kutatua tatizo lazima ujue kiini chake. Vinginevyo baada ya miaka kadhaa tutakuwa na tatizo hilihili.! Hayo matatizo yaliyoorodheshwa na Mr. Hassan ni sawa lakini pia uchunguzi ufanyike ujue kama ni kushindwa kazi kwa kitengo husika au vinginevyo. Hii ni kwasababu kama ukitaka kupunguza tatizo kwa kuongeza kodi kama alivyo dokeza boniface ni kuwaadhibu wananchi kwa uzembe wa hao wafanyakazi husika.

Tatizo kubwa ni kwamba mimi naona serikali imerelax na haino ni kama jambo la emergence!! kama wanaweza kutafuta fedha za uchaguzi kwanini usiweze kuwa wabunifu kwa kiasi hicho hicho kutafuta fedha za kuongeza na kuboresha miundo mbinu bila kumuumiza mtumiaji??


Serikali inaacha masuala ya msingi na kukimbilia masuala yasiyo na msingi kabisa. Huu mwenendo ni wa kuhuzunisha sana.


 

 
     

Abdallah Hassan  : Tuesday, May 18, 2010    
 

Wanachama wa TAKNET




Leo nimekutatna na presentation ya Eng. Charles Z. Wihenge aliyoitoa kwenye moja ya mijadara ya kisera (policy dialogue) iliyoandaliwa na ESRF mwaka 2007. Imenivutia nimeona niwadokezee japo kwa ufupi mawazo yake kuhusiana na matatizo ya usafiri katika miji yetu. Matatizo anayoelezea mengi yameishatajwa na wachangiaji waliotangulia lakini pia alishauri  jinsi ya kutatua matatizo hayo.



Eng. Wihenge ameorodhesha matatizo makubwa ya usafiri katika miji yetu kuwa ni:



   Barabara kujaa mno (Congested roads)



   Upungufu wa mabasi na aina mbaya/ isiyofaa ya mabasi ya umma (vipanya)



   Ukosefu wa uzoefu na utaaalmu  wa shughuli ya usafirishaji – upande wa wasafirishaji,



   Kutofuatilia kwa makini viwango vilivyowekwa



   Udhaifu katika kusimamia taratibu na sheria zinazosimamia matumizi ya barara



   Tabia mbaya iliyojengeka miongoni mwetu ya kutofanya marekebisho/ matengenezo na hapa naamini ni matengenezo na marekebisho ya barabara na miundombini mingine lakini pia na magari yatumiayo  hizo barabara.



Inaendelea hapo chini:

 
     

Abdallah Hassan  : Tuesday, May 18, 2010    
 

Imeanzia hapo juu:



Ili kuepuka matatizo hayo anashauri mambo mengi miongoni mwayo ni:


       Kuanzisha/ kutengeneza barabara zingine ili kupunguza msongamano wa magari


   Kuondoa kabisa katika maeneo ya mijini mabasi madogo (vipanya) na kuleta mabasi yenye uwezo wa kubeba abiria wengi


   Kuanzisha matumizi ya miundombinu ya reli zilizopo (Kituo kikuu cha reli,  Ubungo, tabata vingunguti n.k )


   Kuanzisha usafiri wa boti katika pwani has za Dar es Salaam (bunju, book, wazo, tegeta, mpaka masaki)


   Leseni za kuendesha biashara ya usafirishaji zitolewe kwa watu wenye elimu ya usafirishaji au wenye uwezo wa kuajiri wataalamu wenye sifa


   Viwango virasimishwe na kuongezwa kwenye sheria husika


   Na watanzania waelimishwe umuhimu wa kufanya matengenezo/marekebisho mara kwa mara


Anasisitiza kwamba majukumu yote haya ni ya wabia wote, ikiwa ni pamoja na Serikali (kuu na serikali za mitaa), umma kwa ujumla pamoja na taasisi za kiserikali kama vile SUMATRA na taasisi za binafsi. Umma unatakiwa kuzingatia sheria na taratibu za matumizi ya barabara (habari za kutanua barabarani hazitakiwi), wamiliki wa vyombo vya usafiri waajiri wafanyakazi wenye sifa za kuendesha vyombo vyao na pia Taasisi husika hasa SUMATRA inapaswa kusimamia kwa karibu matumizi mazuri ya usafiri wa umma.




Yameshasemwa mengi, na mataizo pamoja na ufumbuzi unajulikana, tatizo ni nini? Upungufu wa pesa au mipango mibaya, ukosefu wa utaalamu, kukosa uzalendo, ufisadi, au nini?




Jioni njema




 

 
     

boniphace makene  : Monday, May 17, 2010    
  ndugu zangu vipi kuhusu hoja ya kupandisha kodi kwa magari yanayoendeshwa jijini hapa ili walau kupunguza msongamano huu_  
     

Rah Kachwa  : Monday, May 17, 2010    
  Pia iwekwe by-law na halmashauri za manispaa  na jiji la dar kumlazimu kila anayejenga nyumba mf ghorofa aweke sehemu ya maegesho ya magari (parking). Hii itasaidi kupunguza msongamano wa magari, kwani kwa sasa watumiaji wa majengo mengi wanatumia barabara kama 'parking'
Nimeona wiki iliyopita kikao cha viongozi wa jiji kikipanga kupanua barabara ya Ali hassan Mwinnyi. Ni hatua nzuri, lakini katika kupunguza msongamano inabidi pia kujenga 'fly-overs' (it is a fact that to improve a slow process as a whole that has bottleneck stages, you need to add ingredients that will catalyse and improve the speed of the bottleneck stage).
Suluhisho lingine ni kuboresha usafiri wa umma ili kupunguza watumiaji wa magari binafsi.

Rah Kachwa (Dsm, Tz)
 
     

Rah Kachwa  : Monday, May 17, 2010    
  Pamoja na hatua mbalimbali, pia barabara zinapojengwa zikiwe na miundombinu mingine kama mitaro na mifereji ya kutosha ili kusafirisha maji kipindi cha mvua.
Uamuzi wa Chuo kikuu kuwaruhusu 'wawekezaji' kujenga shop mall ya mlimani city (japo sio lengo la uanzishwaji wa UDSM, na pia 'wawekezaji' wamejenga maghala badala ya majengo yaliyokusudiwa) ni ushahidi tosha kuwa 'decentralisation' of the Dar business centre is one viable solution to curb the disgusting dar queues.

rah kachwa (Dsm, Tz)
 
     

Rah Kachwa  : Monday, May 17, 2010    
  Mimi nakubaliana na Nyangubho Nyega hasa katika umuhimu wa kufanya kazi kwa masaa zaidi. kwa mfano uwekwe utaratibu wa kufanya kazi kwa masaa 24, yaani ziwekwe shift 3 (eg saa 1 mpk saa 8, saa 8 mpk saa 4 usiku, na saa 4 usiku mpk saa 1 asbh).
Pia ifanyike kutawanya ofisi za umma kama wizara kutoka maeneo ya Posta na kwenda maeneo tofautitofautiya nje ya mji  kama Kibamba, Kongowe, Boko nk).
Pamoja na hayo barabara za mitaa(feeder roads) ziboreshwe, hizi zitapunguza msongamano kny barabara kuu. Pia barabara mbadala ziongezwe na kuboreshwa kwa mfano barabara inayotoka ubungo maziwa kupitia kigogo-jangwani mpk kariakoo ingejengwa kwa kiwango cha lami. Pia ichongwe barabara ya kutokea sam nujoma, sinza,mwananyamala, hananasif mpk upanga (suluhisho la muda mfupi)

Rah kachwa (Dsm)
 
     

Rah Kachwa  : Monday, May 17, 2010    
 

Today, Dar es Salaam, a home to nearly four million, plus 120,000 vehicles, is facing serious traffic jams, painting a gloomy picture to the future of Tanzanias commercial and economic hub. For instance, motorists as well as passengers spend about 49 percent of their working hours on the road as they struggle with the rapidly growing traffic jams. To motorists, about 40 percent of the fuel they consume is spent on traffic jams, adding costs to the pockets that are already weakened by surging pump prices.According to a survey conducted by the Confederation of Tanzania Industries (CTI) in 2008, traffic jams dent up to 20 per cent of annual profits of the citys businesses. Dar es Salaam Rapid Transit (Dart) Agency, estimates that about the city economy loses Sh4 billion daily a situation that brings together annual losses at Sh1.44 trillion($1billion) . While the problem of congestion affects all sectors of economy, companies that deal with the supply of fast moving consumer goods such as beverages, edible oil, bread and soap constantly find it very hard to timely make deliveries, incurring extra costs in the process. (SOURCE THE SUNDAY CITIZEN)

 
     

Omari Mwinyi Khamis  : Sunday, May 16, 2010    
 

This story although it comes from ippmedia of  16th May is very common.We are at the sametime beign informed that there are around 380,000 motorist in the country but I wonder how many of these motorists are living in Dar es Salaam.Let us say 250,000 motorists are operating daily in Dar es Salaam and these can contribute just 1000 Tz.Shilling  since they are going to be caught in the installed road camera what a big daily income for the Dar es Salaam city.Just imagine the swelling of income in one month and in one year.We could sufficient money to pay for the camera installation,the electricity the cameras will be using and improve our roads in Dar es Salaam and even buy modern buses so that we can forbid the operation of Daladala buses in the whole city and its surroundings.

“But, surprisingly, the two friends who set out from two worlds apart, Mbezi Beach and Johannesburg, arrived at their common destination at the same time.

William says he was caught up in the deadly traffic jam that forced him to spend three hours on the route that covers just approximately 35km.

William is among four million residents of Dar es Salaam city whose biggest worry is the rapidly growing traffic jam, caused mainly by dilapidated infrastructure and poor city planning.”

 

If one spends 3 hours with engine on for just driving 35km that requires only half an hour driving it means the engine will be at a standby for almost 2 hours and 30 minutes.We can calculate how much CO2 gas that cars polluts the air and what is the cost of petroll.People who are used to spend 39,000 Tsh for  30 litre petroll are now forced to pay 51,000 Tz.Shilling to buy the same amount of 30 litres of petroll. The trafic jam is contributing to such expenses and destroys the home economy of individuals,that of the government and increase poverty.

We pay the price of poor planning!Still we don’t learn from our mistakes from Dodoma that we have the airport almost in the centre of Dodoma.We expand the Dar es Salaam aiport towards the centre of Dar es Salaam instead of building a new airport away from Dar es Salaam.Have we forgotten the aeroplane accident that occurred at the Amsterdam Airport(Schipol airport)  few years ago! I was lucky that I was not there since I lived at Amstelveen just outside the airport where the plane crushed into buildings.

Dr.Khamis

Sweden

 

 

 
     

Omari Mwinyi Khamis  : Sunday, May 16, 2010    
 

Thanks Mr. Nyenga for you good ideas as applied in China and Japan but the population of Dar es Salaam does dot resemble that of for example Tokyo . However, what we can do is to close the core of Dar es Salaam from those who just roam about to cause a traffic jam by installing several traffic cameras and fees like in London. Car plate numbers could registered from 7.am to 3pm in areas from Jangwani-to Kivukoni-State House-Tazara Railway Station and Dar es Salaam harbour.These registered car have to pay 1000 Tz.shillings every time they are registered per day in that zone.There should not be Dala buses in this zone.

We can make most of the roads in this zone as one-way roads.We must remember that soon we will have a similar air condition like Athenes in Greece.The CO2 gas will pollut the air in Dar es Salaam since we have along que of cars that have their engine one while waiting to proceed driving.This is a health problem and economic problem.Therefore we have to make a campaign of advising the drivers to switch of their engines while waiting in a que in order to minimise the emmission of CO2 gas.

I still insist that the government could move its offices oustide Dar es Salaam in a scattered way and build small self suffient communities with wide roads and all required ficilities.We must have a broad thinking.

As I understand a donor country had an offer of building a new Dar es Salaam about 10 years ago.Had we accepted that offer we would have avoided the situation we are in today.Now who is to be blamed the Dar es Salaam City Council or the government?

We are now in this mess and we have to go through it and pay the price.However, there is still a chance of minimizing the cost of building fly overs since we have enough land and a long coast line.

Dr.Khamis

Sweden

 
     

Lonyori Kisota Laizer  : Saturday, May 15, 2010    
 

Mr.Maro,ni dhahiri kwamba sote tunafurahia maendeleo,na msongamano wa magari ni ishara ya kukua kwa uchumi.Lakini niulize kama tutakubaliana kubaki katika hali hii,  je si vema kila jamii wa eneo husika wajipange vizuri kwani pindi anapompata mgonjwa au dharura yeyote inayohitaji haraka itawawia vigumu?Serikali wakubali gharama na kuondoa kero za msongamano wa magari.

 
     

Jacks Meena  : Saturday, May 15, 2010    
  Yes,
Talking of Msongamano wa magari and the government that goes to bed by 6.00 p.m like kuku wa kienyeji, leaves much to be desired! The same magari are a good source of income on the part of the government- import and custom duties; fuel; spares; kitu kidogo kwa police force; employment opportunity for thousands of people and their families.......And you have TANROADS, Municipal Councils, the whole government seated in Dar not doing anything to that effect.

Sasa hapa wa kulaumiwa nani? Anaye agiza gari kujikwamua na adha ya usafiri Dar es Salaam au serikali iliyoshindwa kuweka miundombinu imara? The other good thing about the people of Dar is that they live kwa mazoea- they don't view foleni barabarani as a problem caused by irresponsible government but rather the many wananchi who have opted for private cars! Thus the solution to that is to wake up at 4.00 pm in the evening and start hitting the rod.

And at 2 p.m after luch everyone is dozing and thinking of hitting the rod again. So if your organisation has business transactions with firms in the US or Canada- at a time they want to strike good deals, your office is already closed!
 
regards,
 
Meena.
 
     

nyangubho nyega  : Saturday, May 15, 2010    
 

Hello ndugu Maro.

Swala la msongamano nini kifanyike nadhani tufate ule utaratibu uliowekwa wa maroli toka mikoani kuingia mjini kuanzia saa 3 asubuhi, vivyo hivyo iwepo ratiba ya magari mengine kuanzia mf. T.000 AAA- T.111 BBB ndio zitaruhusiwa kuingia na kutoka mjini kuanzia saa12 asub hadi saa 8 mchana. Na gari number mf.T.111CCC- T. 222DDD zitaruhusiwa kuingia kuanzia saa9 mchana hadi saa 2 usiku, na hizi zote ni kwa siku moja tu kwa wiki mf. J'3. Hivyo hivyo kwa number zingine kwa wiki nzima.


Hii itasaidia wengi kufanya shughuli kwa muda maalum na kwa haraka. Mf daladala zitaoperate kwa haraka bila kukata route wala kuendesha rough kama tulivyozoea.Uzuri ni kwamba data zipo za idadi ya magari, swala ni kupanga ratiba kulingana na gari ilisajiriwa kwa dhumuni la huduma gani.


Pia itasaidia huduma hasa za kibiashara kufanya kazi hadi usiku kama nchi zilizoendelea. maana si lazima shughuli zooote zifanywe mchana, ni ngumu sana hasa nchi kama yetu yenye miundombinu finyu. Ni vizuri kuwa na ratiba kusimamia,na kuifata.


Hii ni njia mojawapo ambayo imetumiwa na nchi kama China na Japan wakati wakijipanga kuongeza barabara za juu na train za chini.


Angalizo: Gari kama za Jeshi, Misafara ya wakubwa, ambulance, fire na dharula za watu binafsi zitakuwa na special consideration. Pia ulinzi kwa raia na mali zao lazima uimarishwe mf.kuwepo na police patrol zidi ya majambazi wanaopora magari .


 
     

Omari Mwinyi Khamis  : Friday, May 14, 2010    
 

Assalaam Aleykum vijana.Nakumbuka nilipokuwa ninasoma Chuo Cha Maji Dar es Salaam, huko Ubungo kulikuwa hakuna shida yoyote ya msongamano wa magari.Mabasi yalikuwa yakienda kila robo saa kutoka Kifukoni(sasa hivi kuna soko la samaki) mpka Chuo Kikuu bila ya shida yoyote.Kweli magari wakati huo yalikuwa si mengi sana.

Kitu ambacho serikali yetu kilikosea ni kuanza kuvunja nyumba na kupanua barabara na kupata gharama ambazo si za maana.Serikali ingewacha mji wa Dar es Salaam kutoka Stata House mpaka Magomeni mapipa kama vile vile ilivyukuwa zamani.Sehemu hii ingeitwa “mji wa zamani” ili vizazi vijavyo vione historia yetu.Mfano Stockholm, Sweden, kuna Old Stockholm ambayo ni mji wa zamani na umeachwa vilele na njia zake nyembamba ili kuhifadhi historia ya mji.

Serikali ingelijenga mji mpya wa Dar es Salaam kati ya Ubungo na Morogoro-na Bagamoyo na kujenga njia pana kama zinavyotakiwa.Kila njia ingelikuwa na sehemu nne na sehemu ya tano ya baiskeli na ya sita ya watu wa miguu.Mji huu mpya ungelisambazwa na kila eneo moja lingekuwa na soko,maduka,hoteli,shule na hospitali.Pia wizara za serilkali na ofisi za kampuni kadhaa zingelisambwazwa ili kusiwe na msongamano wa magari wakati wa asubuhi na pia jioni watu wanapomaliza kazi.

Ilyobakia sasa ni kuzifanya barabara kadhaa ziwe na “fly over”.Barabara zigengwe juu ya barabara nyingine hususan barabara ya Morogoro kupitia jangwani na magomeni mapipa mpaka Ubungo.

Kama tumeeza kujenga Dodoma mpya ni kitu gani ambacho kilituzuia kujenga Dar es Salaam mpya?

Dr.Khamis

Sweden

 
     

boniphace makene  : Friday, May 14, 2010    
  Ndugu Maro, nakubaliana na wewe kuwa msongamano kama dhana si tatizo. Ni ishara ya kutanuka kiuchumi na kukua.
 
Lakini fikiria kama msongamano unakwaza mtu kutoka eneo moja kwenda nyingine, je, hapo huoni unasababisha mkwaruzano hasa inmapotokea kila mmoja anataka kutoka alipo na hivyo kujifunga kabisa?
 
     

Festo E. Maro  : Friday, May 14, 2010    
 

Msongamano wa magari hapa jijini ni taswira iliyopo kwasasa ikionyesha ukuaji wa kipato kwa wakazi wa Jijini. Msongamano si tatizo ila, tatizo ni mwendo au speed ambayo haya magari yanaenda na mda unotumika kufika sehemu unayoenda. Ukiangalia idadi ya magari yaliyopo hapa jijini sidhani kama yanafikia yale yaliyopo Nairobi. Taifa linapoteza rasilimali nyingi sana kwa hili tatizo la muda unaopotea barabarani na malighafi ya petroli/dizeli na oil za kulainisha vyuma vya magari kwasababu vyote hivi tunaagiza nje. Tunatumia hifadhi ya fedha benki kuu kununua hizo bidhaa.


Tatizo ni hii miundo mbinu yetu ambayo inajengwa katika mtazamo mdogo sana. Kisingizio kikubwa ni gharama. Inastaajabisha kuona baada ya kujenga hiyo miundombinu miaka mitano baadae wanakuja kupanua kwa gharama kubwa zaidi ikiwa na kulipa fidia kwa kuvunja majengo ya wananchi ambao awali hawakuwepo. Swali kwa hawa viongozi husika ni lini hizi gharama wanadhani zitapungua ili waweze kujenga miundo mbinu yenye kukidhi maendeleo ya nchi kwa miaka 30 au 50?kwa kifupi hamna na wasitegemee hilo. Barabara zetu hizi zingejengwa katika huo mtazamo hili tatizo la msongamano ambao hauna tija lisingekuwepo.

Chakufanyika sasa ni wao kuingia katika gharama ambazo walikuwa wanazikwepa miaka iliyo pita kwa kuhakikisha feeder roads zote zinajengwa katika kiwango cha lami.

Serikali ianze kufikiria kujenga satelite cities ili kupunguza muelekeo wa magari yanayoenda posta au katikati ya jiji.


Flyovers wafikirie kujenga ila ziwekwe katika sehemu korofi sana. 

 
     

  This topic has been closed. You can only view comments!  
     

 

 

  ESRF
  Tanzania Development Gateway
  Tanzania Online
  Government of Tanzania
  United Nations (UN)
More»
 
v  
v TOP CONTRIBUTORS
  Omari Mwinyi Khamis(156)
  Festo E. Maro(69)
  Abdallah Hassan(49)
  japjet Makongo(30)
  Kabuje Furaha(26)
   
All Contributors»



 
Tanzania Knowledge Network (TAKNET) Platform is supported by The Government of United Republic of Tanzania,
United Nations Development Programme (UNDP) and coordinated by Economic and Social Research Foundation (ESRF).


Disclaimer | About Us | Feedback | Membership | Contact Us | Admin
© 2015 Economic and Social Research Foundation. All Rights Reserved.