A joint initiative by the United Nations, The Government of Tanzania and The Economic and Social Research Foundation  

A platform for professionals and experts to meet, share and exchange experiences
Username >

Password >

Forgot | Change Password? Register! Home
Topic : Vifo Vya Akina Mama Kutokana Na Matatizo Ya Ujauzito(Maternal Mortality) ni tatzo kubwa Tanzania : Nini kifanyike kutatua tatizo hili?*  
 

Mbali na jitihada za dhati zinazofanywa na serikali yetu kwa muda mrefu kutatua tatizo la vifo vya akina mama kutokana na matatizo ya ujauzito (martenal mortality), takwimu za karibuni zinaonyesha hali sio nzuri kwani vifo vya akina mama vinaendelea kuongezeka kila mwaka. Bila ya mi ...Click here to read more

     
Comments From TAKNET Members
Josephine Lemoyan  : Monday, November 22, 2010    
  Dr Khamis na ndugu wadau washiriki wa mdahalo huu

Nakushukuru Doctor kwa mawazo yako... Lakini mchokozi kweli kweli. Tufunge wodi zetu? Nadhani hapana ila tujiulize kama kweli kwa dhati tunakusudia kama Taifa kupunguza vifo vya wanawake wajawazito na vile vinavyotokana na uzazi. Je vipaumbele vyetu ni nini na tumevifanyieaje kazi? Mimi ni mgeni kidogo katika sekta ya afya ndiyo kwanza nimeanza kuifanyia utafiti kidogo kidogo na kujihusha na interventions kwenye sekta hii nami pia najifunza.

Kwa kweli upo utaratibu wa kuweka vipaumbele vya maendeleo katika nchi yeyote ile dunia. Nimepitia miongozo kadhaa ya Wizara ya Afya na niumekuta masuala ya RCH yamepewa kipaumbele na uzito mkubwa kama vile katika National Package of Essential Health Interventions na katika Mpango wa Maendeleo wa Afya ya MSingi - MMAM au Primary Health Services Development Programme- PHSDP 2007-2017. Ukurasa wa 38 hadi 41 unazungumzia tatizo hili na pia katika appndicies kuna bajeti kubwa iliyopendekezwa katika eneo hili la RHC  kwa miaka 10  ni Tshs 2,385,485,000,000. Mpango mzima wa MMAM inatarajiwa kutumia kama trillioni 11.8 kama fedha zilizokusudiwa zitapatikana.

Nikiangalia shughuli zilizopangwa ili kufikia malengo tuliyojiwekea najiuliza je ni kweli kazi zilizoazimiwa zitatufikisha kwenye lengo? Kwanza Objective (lengo/lengo kuu? au dhamira- ni kupunguza MM from 578 to 220 per live birth by 2012. Baadhi ya shuguli katika Taget years (mwaka wa kwanza hadi mwaka wa kumi) ni:
- kufundusha watoa huduma kuanzia 2,000 (mwaka wa kwanza na wa pili) kuhusu maternal and new born care (na kazi hii inaendelea kwatika miaka inayofuatia ikizidi kupanda hadi 2,200 (target yr 3 and 4); 1,800 (target year 5 and) na 1,000 kwa yrs 6/7 na 1,000 yr 9 &10
- Kufundisha wakufunzi miambili-miambili  kwa miaka hiyo hiyo lakini target yrs 9 &10 - shughuli ni ya ufuatiliaji i.e. follow up of 50% of traines service providers in all regions.
- Seti nyingine ya shughuli zitakazotumia bajeti iliyowekwa ni kununua vifaa vya RCH kwa ajili ya vituo 60 (yr1/2; same yr3/4 na same yr 5/6)
- Halafu kufanya ukarabti wa vyumba vya upasuaji, labour wards na RCH clinics ikiwa ni pamoja na nyumba za wafanyakazi katika vituo 40 (yr1/2) halafu same activities kwa miaka inayofuatia na ikifika target yr 7/8 basi ujenzi wa vyumba vya upasuaji, labour wards, clinics na nyumba za wafanyakazi zitajengwa katika vituo hivyo vipya 52.
- Kazi nyingine ni kununua ambulance, kuanzisha Community Health workers, na mengine mengine ikiwa na kuimarisha huduma za TBAs zoezi ambalo kwa mtazamo wangu limepewa uzito mdogo.
- Naomba nisahau pia kuna mpango wa kutoa vocha ya doti moja ya khanga kwa akina mama wajawazito ili kuwavutia wahudhurie kliniki na kuwafanya waende kujifungua katika vituo vya kutolea huduma ya afya (idadi ya wanawake watakaonufaika na motisha hii ni 1.4 milion yrs1&2; same number yrs 2/3 inaongezeka kufikia 1,450,000 yrs 4&5 na 1.5 million yrs 7&8 na mwishowe inaongezeka kwa elfu hamisni katika target years za mwisho.

Nikiangalia mpango huu wa kimkakati najiuliza kwa kufanya hivi tutapunguza vifo vya wanawake wakati wa uzazi?

Duru ya kwanza ya utekelezaji ni ya miaka mitano 2007-2012 najiuliza tupo wapi kwa sasa maana muda uliobaki nu takriban mwaka mmoja tu kwani ni karibu tunaanza mwaka wa 2011.

Nikirudi katika swala lako la kufunga mgodi, naona tusifunge lakini wewe na mimi na watafiti, na wadau kwa ujumla hebu tuichunguze MMAM vipi imeanzaje, iko wapi sasa na ianelekea wapi? Vile vile nadhani juhudi za dhati za kushambualia hili tatizo la vifo vya wanawake vinavyotokana na ujauzito toka kila upande liendelee.

Kwa uelewa wangu wa kiasi, kuna maeneo yanayofanya vizuri na yale ambayo yana matatizo sugu. Je tumejifunza nini kutoka kwao? Ni uzoefu upi unaweza kutumika sehemu nyingine? Kama haiwezekani basi sehemu zanye matatizo sugu zishughulikiwe vipi? Kwa mtazamo wangu hakuna jibu la jumla jumla kuhusu tatizo hili na matatizo mengine ya kijamii!

Wasaalamu

Naomba kuwasilisha kwa sasa ...
 
     

Omari Mwinyi Khamis  : Friday, November 19, 2010    
 

Ndugu Josephine maelezo yako ni mazuri mno na twashukuru kwa utafiti wako.

1. Wakunga wawili ambao wanatumika katika shift moja hawawezi kuwazalisha wajawazito 60 hata wakiwa na miujuza ya aina yoyote. Mimi mwenyewe nimefanya kazi kiwandani na nilifanya kazi miaka 25 katika migodi ya Sweden na nilitumia hekima hii ya ”shift”.Huwezi kuzalisha mgodi wowote ukiwa na wafanyikazi wa kuchima wawili tu katika shift moja.Ni afadhali kufunga mgodi huo ama sivyo lazima uajiri wachimabji wanaohitajika kwa kila shift ili uzalishaji wa madini uwe wa faida.

2.Vifaa vya uzalishaji ni vitu muhimu sana.Hapa pia nato mfano wa uchimaji madini.Kama mgodi hauna mashine za kutoboa ili kuweka baruti wala mashine za kuchukuwa madini au mawe ya madini yanapulipuliwa, wala mashine za kusaga mawe mgodi huo utapata matatizo ya daima. Hii ndio sababu ya wodi za uzazi na pia hospitali zetu zina matatizo daima.

3.Kwa nini hatufungui wodi chache za uzalishaji na ambazo zitakuwa na wakunga kamilifu na vifaa bora ambavyo ni vya kisasa.Tufunge wodi za uzalishaji ambazo ni matatizo kwa serikali na usumbufu kwa wananchi.

 

Dr.Khamis

Sweden

 
     

Josephine Lemoyan  : Friday, November 19, 2010    
 

Asante sana kwa dondoo zinazozidi kutuimarisha katika fikra na baadaye sisi tunaojaribu kubuni mbinu za utatuzi kwa matendo tunaweza kupata mapya ya kufanyia kazi.  Pia naomba nitoe shukrani kwa TAKNET kwa kupokea mawazo angalau kidogo niliyoweka katika sehemu ya maono nia yangu ilikuwa kupost kwenye mnyororo wa mjadala uliokuwa ukiendelea lakini nilikosea kidogo lakini angalau kuna response hili ni la muhimu. sasa tuendelee!


Kubwa katika mchango nilioutoa ni dhana ya uwajibikaji (accountability).


Dhana hii inahusiana sana na hali ya mifumo ya ndani ya taasisi na hapa katika utoaji wa huduma ni taasis inayouhika kutoa huduma ya uzazi na afya ya mtoto. Ukiangalia mfumo ulivyokaa utakuta kuwa kuna mambo mengi sana ya yanayokinzana. Hapa watoa huduma binafsi (nesi au daktari n,k,) ni sehemu ya taasisi lakini mifumo iliyopo haiwawekei taratibu za mahusiano ya uwajibikaji.

1. Suala la idadi: Kabisaaa kaka Abdallah - idadi ya watoa huduma haina uwiano hata kidogo na wale wanaohitaji na kuipokea! Katika utafiti mdogo tulioufanya (si kwa sababu hali haijulikani lakini kwa sababu ya kuweka hoja kitaalamu); tuliona katika shift moja ya hospitali fulani, kuna nesi wawili katika wodi ya wazazi. Walitakiwa kati ya saa mbili asubuhi na saa nane mchana wazalishe wanawake 60 - inaingia akilini? Hata kama wangekuwa na utashi wa namna gani si rahisi hawa wakunga wawili kuwahudumia wanawake wote hao.

Swali: Iwapo MMR - Maternal Mortality Rate: ni moja ya vigezo vya maendeleo ya milenia ambavyo tunatakiwa kuvishughulikia nini kimefanyika mpaka sasa hivi ili kuleta angalau uwianao wa watoa huduma kwa wataje wao?

2. Vifaa: je ni nani mtoa vifaa vinavyo hitajika katika utoaji wa huduma ya afya? - Simpo- Ni MSD kulingana na mahitaji ya kituo cha kutolea afya kinachohusika. Sasa angalia - Je utaratibu wa kupata vifaa hivyo ukoje? Hapa ndio utachoka. Nadharia iliyopo katika mfumo wa kupanga mipango na bajeti ya kituo cha kutolea huduma kwa siku hizi ni 'decentralised' Hivyo kamati ya kituo inatakiwa kupanga mipango na kuiwasilisha katika ngazi za juu kwa ajili ya kuunganishwa ili kupata mapango mmoja wa wilaya. Je nini kinafanyika kwa vitendo? Wananchi na structuers zao (nyingine wamezichagua wao wenyewe wananchi) hawajui wajibu wao na majukumu yao. Vile vile kuna mkanganyiko wa sera/miongozo ambayo kwa mdau wa kawaida; mtumia huduma ya kituo cha afya hajui wapi pa kushika (overlapping and conflicting regulatory frames). kwa kukosa miongozo na taarifa sahihi baadhi ya mifumo imebadilika lakini sehemu nyingine kuna mifumo mingi ambayo bado wananchi wanaitumia bila kujua nani anawajibika wapi na kwa namana gani. Kutokana na mkanganyiko huu wote tunalia lakini kilio chetu hakifiki mbali kinakwama katika mkanganyiko huu!


2b. Nikirudi kwa mtoa vifaa yeye anatoa kulingana na mahitaji! kaletewa idadi na aina ya vifaa anatoa. Hapa sasa kuna mambo nani alipanga na kuagiza vifaa? Ni priority/kipaumbele cha nani kuleta stethoscope na sio mashine ya blood pressure?  Kwa vile mambo mengi yalioandikwa kwanye miongozo ni nadharia, basi sisi tulijifunza katika wilaya hiyo ya utafiti kuwa mipango hupangwa mezani katika ngazi ya wilaya. Hakuna kipaumbele cha kituo cha afya xx kinachozingatiwa as such. Kwa hiyo mara nyingi hata watoa huduma hulalamika jamini tumeletewa kifaa x wakati mahitaji yetu ni kifaa z! Usiulizie kiwango cha ubora ndo utachoka!


3. Tija... Ndugu zangu hili linamgusa kila mtu. Najiuliza zile PAY REFORMS zimeishia wapi? - Najitahidi nisiseme nauliza jibu!


4. Suala la Umasikini ni pana na mimi naomba niliangalie tena ni suala la kimfumo. Je tuna utashi wa kutosha kisiasa na kijamii kutatua tatizo la ukosefu wa chakula, fedha, viwanda, wataalamu wenye utashi wa kitaalamu na wanasiasa wanye utashi wa kisiasa? Tanzania si nchi masikini. Tukikubali kuitwa masikini tutazidi kudidimia na tutakuwa masikini kweli kweli. Tuna ardhi nzuri na ya kutosha, tuna maji, tuna mvua, tuna raslimali nyingine kama madini. Na kubwa zaidi tuna WATU!! Tukipania tunaweza kuondoa 'UMASIKINI' WETU SISI WENYEWE! Tukipania tunaweza kuboresha huduma za kijamii. Tukipania tutakomesha vifo vinavyotokana na uzazi na vile vya watoto chini ya miaka mitano.

Naomba kuwasilisha na tuendelee kujadili.


Wasalaam!

Josso

 
     

Omar Mohamed Said  : Friday, November 19, 2010    
 

Kwa upande wangu napenda kuchangia kama ifuatavyo:-

Nafikiria kwanza kabla ya kuona tatizo hili linasababishwa na uwajibikaji wa watoa huduma ni vizuri kuona kwamba jee! mfumo uliopo wa huduma za afya unakidhi haja na matarajio ya umma. Sekta ya afya kwa jumla ukiangalia utaona kwmba haina vifaa na vitendea kazi ambavyo vinatosheleza katika  kutoa huduma maridhawa.


Pili  kwa upande wa watoa huduma jee  idadi yao  ina uwiano mzuri  kulingana na wateja wao. Tukiangalia kisheria watoa huduma wanalingana  vizuri na wateja wao. mtoa huduma mmoja anaweza kuhudumia wateja wangapi kwa kipindi- lipo suala la kuchoka na kushindwa kutoa huduma ipasavyo wakati inapotokea wazazi wawili au watano wanapotaka kujifungua wakati ndani  ya wodi  kuonekana kuwepo kwa  watoa huduma wawili au watatu tu.


Suala ya tija ya kazi ni jambo jengine na la msingi jee  mafao na mishahara ya watoa huduma imeboreshwa  kulingana na hali halisi ya nchi na pia ukilinganisha na  sekta nyengine kama ya siasa.

Suala la umasikini na afya mbaya ya wabebaji mimba nalo ni suala la  kuangaliwa ipasavyo. Watanzania

Kwa upande wangu napenda kuchangia kama ifuatavyo:-

Nafikiria kwanza kabla ya kuona tatizo hili linasababishwa na uwajibikaji wa watoa huduma ni vizuri kuona kwamba jee! mfumo uliopo wa huduma za afya unakidhi haja na matarajio ya umma. Sekta ya afya kwa jumla ukiangalia utaona kwmba haina vifaa na vitendea kazi ambavyo vinatosheleza katika  kutoa huduma maridhawa.


Pili  kwa upande wa watoa huduma jee  idadi yao  ina uwiano mzuri  kulingana na wateja wao. Tukiangalia kisheria watoa huduma wanalingana  vizuri na wateja wao. mtoa huduma mmoja anaweza kuhudumia wateja wangapi kwa kipindi- lipo suala la kuchoka na kushindwa kutoa huduma ipasavyo wakati inapotokea wazazi wawili au watano wanapotaka kujifungua wakati ndani  ya wodi  kuonekana kuwepo kwa  watoa huduma wawili au watatu tu.


Suala ya tija ya kazi ni jambo jengine na la msingi jee  mafao na mishahara ya watoa huduma imeboreshwa  kulingana na hali halisi ya nchi na pia ukilinganisha na  sekta nyengine kama ya siasa.

Suala la umasikini na afya mbaya ya wabebaji mimba nalo ni suala la  kuangaliwa ipasavyo. Watanzania ni masikini katika nchi yenye raslimali za kutosha zisizotumika ipasavyo. Mfumo wetu wa maisha ya kijamii ni mbaya. Hatuweki kumbukumbu za kutosha katika ngazi ya shehia au kijjiji kujua kipato cha kila mkaazi na vipi  kuweza kusaidia pale mapungufu yanapoweza kutokezea hasa suala la mahitaji ya lazima.

Nakubaliana na mtoa mada  utoaji ya elimu ya  afya  ni muhimu na lakini yapo mambo ya msingi ya kufuatiliwa kama nilivyoelekeza kwanza ili kuweza kurekebisha hali hii. Ni vizuri kwa watanzania kuweza kuamua kwanza jee tupo tayari kutatua tatizo au tunaimba tu kama  wanasiasa ili kuweza kutimiza malengo yetu kinyume na yale tunayoyasema katika public.ni masikini katika nchi yenye raslimali za kutosha zisizotumika ipasavyo. Mfumo wetu wa maisha ya kijamii ni mbaya. Hatuweki kumbukumbu za kutosha katika ngazi ya shehia au kijjiji kujua kipato cha kila mkaazi na vipi  kuweza kusaidia pale mapungufu yanapoweza kutokezea hasa suala la mahitaji ya lazima.

Nakubaliana na mtoa mada  utoaji ya elimu ya  afya  ni muhimu na lakini yapo mambo ya msingi ya kufuatiliwa kama nilivyoelekeza kwanza ili kuweza kurekebisha hali hii. Ni vizuri kwa watanzania kuweza kuamua kwanza jee tupo tayari kutatua tatizo au tunaimba tu kama  wanasiasa ili kuweza kutimiza malengo yetu kinyume na yale tunayoyasema katika public.

 
     

Josephine Lemoyan  : Wednesday, November 17, 2010    
 

Nimejiunga hivi karibuni katika ulingo huu nashukuru. Ninaitwa Josephine (Josso) na ningependa kuchangia mada hii kama ifuatavyo.

Nafikiri vifo vya wanawake wajawazito ni jambo linaloweza kuzuilika. Moja ya sababu zinazochangia vifo vya wanawake wajawazito na watoto wachanga ni kukosa uwajibikaji wa wale wanaotoa huduma kwa ajili ya Uzazi na Afya ya Mtoto. Nini kifanyike? Hivi karibuni mimi na wenzangu tumeanza kufikiria namna ya kuhimiza uwajibikaji. Na uwajibikaji huu kwenye suala linalohusu mauti ni jambo la kila mmoja wetu. Katika kulitafutia ufumbuzi tumegudua kwamba kumbe iwapo kifo cha mama mjamzito au/na mtoto mfu kimetokea basi lazima wale waliotoa huduma wafanye mkutano kujadili kifo hicho. Mkutano huu unaitwa Maternal Mortality Meeting. Hapa wahusika hujadili nini kimesababisha kifo hicho na kutafuta njia za utatuzi ili kifo cha aina hiyo kisijirudie au kutokea tena.

Utafiti uliofanyika hivi karibuni unaonesha kuwa mikutano hiyo pengine hufanyika katika vituo vya kutolea huduma. Lakini ikifanyika, matokeo ya mikutano hiyo hupelekwa ngazi za juu na hakuna mtiririko wa mrejesho mahususi kwa wadau ikiwa ni pamoja na familia, majirani, kituo cha kutolea huduma, kamati ya kituo husika na bodi ya kituo husika! Vile vile tumegundua kuwa kumbe hata kifo cha aina hiyo kikitokea nje ye kituo cha kutolea huduma k.m. kwa mkunga wa jadi (TBA) au nyumbani maternal mortality meeting ni budi ifanyike. lakini haifanyiki.

Basi sisi kwa kushirikiana na wadau wa afya hapa Mwanza tumejadili na kuandika andiko la mradi namana ya kuwezesha kufanya mikutano hii kuwa effective ndani na nje ya kituo cha kutolea huduma ya Uzazi na Afya ya Mtoto. Tunafikiri tukiwezesha vizuri mikutano hiyo tunaweza kuwashirikisha wadau wote kukabiliana na tatizo hilo kwani mikutano hii itapembue nini chanzo cha tatizo na nani alitakiwa kuwajibika wapi na kwa vipi. Kwa mfano pengine kifo kimetokea kwa sababu ya mama kutojua dalili hatarishi wakati wa uja uzito. pengine alikuwa na dalili hatarishi lakini hakujua kwa sababu hakuhudhuria kliniki. Hatua ya utatuzi itakuwa ni elimu kwa mama, baba na jamii pengine mama kafariki kwa ajili ya umbali toka nyumbani hadi kufika kwenye kituo cha kutolea huduma Utatuzi utakuwa ni namna ya kuimarisha access to repreductive health services. Pengine kifo kimetokea kwa ukosefu wa vifaa muhimu vya kuhudumia, basi machakato wa priority planning and budgeting for health services utafanyika kwenye kituo husika, kuwachukulia hatua wasiowajibika. Pengine sababu ni uzembe! basi hapa ni kasheshe.

Mbinu nzuri za ushauri na uwezeshaji zinahitajika ili kuwezesha wadau husika kuchkua hatua zinazostahili Kama nilivyoanza hapo juu sababu ni nyingi na zinatofautiana. Kwa sababu hii sisi tutatumia case approach ili kukidhi mahitaji yanayotofautiana. Tutatumia sana mbinu ya mawasiliano kwa umma kama Radio, Magazeti na TV kwa ajili ya kupashana habari na kukuza uelewa wa wananchi na wadau kuhusu jambo hili. Andiko la mradi huu wa Accountable RCH Service Delivery ndio linamaliziwa ili kulifikisha kwa wadau wanaofadhili michakato ya uwajibikaji. Nitaendelea kuwapasha matokeo ya mchakato huu na changamoto au mafanikio tutakayoyaona. Naomba kuwasilisha- Josso

 
     

Weston Allan  : Friday, September 3, 2010    
 

Wengi wa wachangiaji wamechangia kwa  usahihi kabisa. Labda niongezee. Tatizo kubwa la Tanzania na pengine la nchi nyingi za Afrika, ni lile ambalo alishawahi kuliandika kwa kirefu, mwandishi wa habari maarufu hapa nchini. Tatizo letu ni Uongozi, uongozi, uongozi. Basi!


Viongozi wetu hawajatoa kabisa nafasi katika kuwekeza kwenye huduma ya afya. Wanachojua wao ni kuwepo kwa zahanati pekee katika kijiji X bila kujali kama kuna wahudumu wa afya au la.


Tembeleeni katika zahanati za vijiji vyetu. Utakuta jengo na mhudumu wa afya mmoja (Medical Attendant). Ukibahatika sana, utamkuta ameongezeka Tabibu mmoja tu. Sasa, kwa mazingira haya utategeaje huduma bora?


Mimi ningeishauri serikali yetu iwekeze katika huduma za afya na vifo vya wajawazito vitakuwa historia.


Frank

 
     

Marjorie Mbilinyi  : Friday, September 3, 2010    
 

Pamoja na kukubali kwamba kuna ukandamizaji hali ya juu kwa wanawake wakati wa kujifungua, ni muhimu kuchunguza zaidi sebabu kiini .. kuanza na mfumo wa sekta ya afya, nafasi ya wanawake wakiwa wafanya kazi au wateja/clients .. na jinsi wahudumu wanawake wanavyo kandamizwa na kunyonywa na mfumo mwenyewe .. pamoja na wafanyakazi wote hasa katika ngazi ya chini -- wanaotoa huduma za kila siku ikiwa usafi pamoja na zote nyingine muhimu


ukimwona mnyonge anamkandamiza mnyonge mwenzake muhimu kuuliza kwanza kwa nini anafanya hivyo badala ya kutambua adui yake ni nani? Kwa kila hadithi mbaya juu ya uzoefu wa uzazi, bila shaka kuna hadithi nyingine nzuri juu ya wahudumu waliosaidia kuokoa maisha ya mama na/au mtoto ..  na wakati huu serikali yetu inakataa kuelekeza pesa zinazotakiwa kwa huduma za afya, na kuhakikisha kwamba pesa zinafika na kunufaisha mgonjwa pamoja na mhudumu wa afya mwenyewe -- na si mikutano, safari za nje, na kadhalika


kama wengine wengi waliotangulia wamekwisha kusema, kiini cha vifo vya akina mama wakati wa mja mzito ni kutokuwa na wahudumu wa kutosha na wenye mafunzo/ staadi inayotakiwa; umbali wa vituo vya afya kwa wanawake; gharama za safiri; gharama za huduma kinyuma cha sheria; kutokuwa na vituo vya kutosha vyenye huduma za emergency obstetricic [sp?] care ..  ki msingi wake serikali yetu haijaweka kipaumbele kwa huduma za afya na hasa afya ya uzazi -- na si serikali tu, hata wanasiasa, hata waBunge, na hasa sisi raia hatujadai uboreshaji wa huduma za afya ya uzazi na kudai haki ya wanawake kuzaa bila hatari ya vifo ..


kilwa mwaka wanaharakati wanaongea juu ya idadi ya wanawake wanaokufa katika uzazi zaidi ya wanawake 25 KILA SIKU .. je waangapi tumeshangaa na kuandika barua kwa wahusika au gazeti? waangapi tumedai ilani ya uchaguzi ya kila chama ieleze mkakati gani kuboresha huduma za afya? au kufanya maandamano?


wape wahudumu wa afya motisha na nyenzo za kufanya kazi zao na heshima inayostahili na watatoa huduma nzuri. Suala ni mfumo, sera na bajeti .. na kimsingi ya yote ni jamii yetu ambayo haithamini ya kutosha maisha ya mwanamke.


Marge

 
     

costa john kanaysu  : Friday, September 3, 2010    
 

Tanzania kama nchi zingine masikini dunian bado ina mambo mengi ya kufanya, lipo la afya,shule na mawasiliano.Tumejikuta katikati ya uhitaji wa mahitaji haya kwa pamoja bila kujali lipi ni bora kuliko jingine na issue hapa siyo matajili kuumiza masikini hapana ni mabadiliko katika kuishi yanayoikabili dunia nzima.



zamani tulizoea sana kupewa huduma bure wengi hawajui sababu,wakati huo nchi yetu kama zilivyokuwa nchi zingine africa hasa za kijamaa zilikuwa zinafaidika na ugonvi baridi kati ya magharibi na mashariki na ili hawa wakubwa wapate wakuwaunga mkono walijipendekeza kwetu, leo haiwezekani.



nini kifanyike sasa? ni vyema watanzania tukabadilika kutoka huko tulikokuwa kuja kwenye karne hii,kama unajua mkeo amekalibia kujifungua weka hakiba na uanze kujua ni wapi mkeo atajifungulia, kama fedha huna sogea kalibu na hospitali za serikali.



pili tuelewe fika kwanza mimba siyo heart attack kwamba inakuja ghafra,unapoamua kuzaa lazima ujue kuna gharama inakuwaje upate hela ya mahali au ya chumba kama ni starehe alafu ukose elfu tano ya faili hospitali tujifunze kuweka akiba sasa hata huko kwenye kata na vijiji dispensary zipo na serikali imetoa vibari kwa wataalamu kuanzisha vituo na dispensary  watu hawaendi wanasubiri wakatibiwe bule mambo haya yamepitwa na wakati hakuna dunia leo ambapo watu wanalala kungoja kupata huduma bule eti kwa kuwa kuna matajili wakubwa au kuna serikali italeta no no no no no no no no no!




TEL 0282540050-OFFICE
0732/0767/0715/0784643322
MWANZA-TANZANIA.

 
     

japjet Makongo  : Friday, September 3, 2010    
 

Sina uhakika kama nitakuwa narudia yaliyosemwa na wengine.


Kimsingi, sababu za ongezeko la vifo gvya akina mama wajawazito zimejika katika umaskini zaidi. Tafiti zinatuonyesha kuwa vifo vingi vinatokea kwa familia maskini na zilizo mbali na huduma. Hivyo ni busara kulichukulia tatioz hili katika awamu tatu..... za muda mfupi, kuhakikisha walio na tatizo kwa wakati huo wanapata huduma bora...pengine hapa ndipo ahadi ya mheshimiwa mgombea kura (mgombania kula) ya kutoa bajaji zinaweza kusaidia, japo kuna uwezekano wa baadhi kushindwa gharama. Pia bajaji hafiki kila mahali..sehemu za milima na visiwa vidogo Ukerewe, na Kilwa!


Pili ni mikakati ya muda wa kati, kutoa elimu ya uzazi, na kuboresha  huduma katika vituo na majumbani, na tatu ni suala al muda mrefu kuhakikisha kuwa kuna mikakati ya dhati ya kusadia jamii kuongeza kipato chao.  Haiwezekani wakina mama toka Lushoto na sehemu zinazotoa matunda kwa wingi wafe wakati matunda yao poia yanaoza bila soko! TUNAHITAJI DHAMIRA YA KISIASA.

 

MAKONGO
 
     

S. Moyo  : Thursday, September 2, 2010    
 

Poleni akina mama kwa kunyanyaswa na wanawake wenzenu. Naamini adui wa mwanamke ni mwanamke mwenyewe.


Hii ni kwa sababu vifo vingi vya akina mama havitokani na matatizo makubwa ya kisayansi ya kitabibu ila usimamizi mbovu, roho mbaya , rushwa na kutojali kwa manesi wetu. Hivi vitimbi ndivyo vilivyopo mahospitalini. Imagine umempeleka mama mjamzito hospitali unaambiwa hutapewa huduma mpaka ukamilishe pesa uliyodaiwa kwa rushwa.

Nenda kasikilize matusi manesi wanavyo tukana wajawazito. Mama akiomba msaada utasikia mfuate huyo aliye kupatia mimba. Mara usitusumbue hatupo kwa ajili yako hapa mara unataka nijigawe ili nimhudumie huyu na wewe nikuhudumie. Nimepate kumsikia nesi akisema kuwa huyu mwanamke asije akatulaza macho. Sisi tumechoka, muache sisi twende tukalale kule tumechoshwa na kelele zake.

Je yote haya yanahitaji mtaalamu. Je hujashuhudia nesi kamsusia mama mjamzito eti tu kwavile hakufuata maelekezo ya nesi labda kwa vile maumivu yamemzuia huyu mama asitende kama alivyoelekezwa. Kuna mengi tu na ya kutisha zaidi. Nimeshuhudia mama mjamzito kaachwa mapokezi mpaka kafariki bila hata kuhudumiwa. Ndugu za dada huyu waliambiwa bila alfu 75 mgonjwa wenu hapati huduma kwa dactari. Wakinamama hawa wakiendelea kuchangishana mmoja hadi mwingine wakimfuata huku hadi kule huko morogoro, mwishowe baada ya masaa karibu nane baada ya pesa kutopatiokana akafariki. Huyu alikuwa muhudumu wa Bar.

Hii ni aibu na inatisha sana kupeleka mjamzito katika hospitalizetu. Na hivi vyote havihitaji utaalamu wa kiwango cha juu. Kwa ukarimu tu, kupunguza rushwa, kutoa huduma ya haraka na kumjali mgonjwa na matakwa yake, vifo vitapungua kwa aslimia 90. Nenda Fast Track muhimbili uone hali ilivyo. Ndipo utagundua kuwa hatuna haja ya kuajiri dactari bingwa maana huku kote hatujafika. Nadhani kunahaja ya kuongeza huduma ya wakunga wa jadi maana hawa huduma yao ni muhimu mno. Wanaupendo na mara kwa mara wamezalisha wajawazito pale manesi wanapo wakataa au kuwa temndea ukatili.

Wanaume wanatakiwa sasa waichukue kazi hiyo maana akina mama hawaoneani huruma. Ndo maana panapo kuwa na mkunga mwanamme akina mama wanamkimbilia na kumganda kama luba.


 


Dr salatiel Moyo Simon Mwakyambiki

 
     

nyangubho nyega  : Wednesday, September 1, 2010    
 

Tunakushukuru muheshimiwa Bariki Kaale.


Mchango wako ni mzuri sana, binafsi ningependa uingie deep zaidi kutuonyesha ni kwa vipi sasa hizo data na tafiti mbalimbali zitasaidia kutafiti na kupunguza vifo vya akina mama na matatizo ya ujauzito, hasa ukizingatia wakati huu ambapo wagombea wetu wanatoa ahadi tele. Mfano mgombea wa ccm ameahidi kupelekea akina mama wajawazito bajaji 400! What is the relationship with Maternal martality? au bora liende!


Naomba mchango wako tena baada ya kupata detailed data za deforestation rate,nguvu za nishati hakuna, are the bajaji a soln for reducing maternal mortality? We need to think twice if this is from national perspective! What should be short/long strategic planning? apart from tree planting and eviction of cattle grazers from water sources.

 
     

senorina kimario  : Wednesday, September 1, 2010    
 

Chanzo cha tatizo hilo ni umaskini na ubinafsi kwa watu wachache wenye navyo wanotumia rasilimali za nchi kwa manufaa yao wenyewe.mfano mzuri ni maeneo ya vijijini barabara mbovu , huduma ya usafiri hamna na watu wanatumia baiskeli kuwapeleka wajawazito kwenye vituo vya afya jambo linalohatarisha maisha yao.mama anapotaka kujifungua mpaka afike kwenye kituo cha afya .inakuwa tabu ndio maana wengine wanajifungulia majumbani na barabarani wakiwa kwenye process za kwenda hospitali


Maoni yangu ni kwamba serikali ni lazima ijenge vituo vya afya huko vijijini ili wajawazito wapate huduma inayowastaili na pia kuwa na madaktari na wauguzi wa kutosha sio wanganganie mijini.pia miundo mbinu kama barabara ni lazima serikali iweke mpango wa kuziboresha ili ziweke kupitika kwa kipindi chote cha mwaka.Serikali ni lazima iipe sekta ya afya kipaumbele na wauguzi wawe naukaribu na wagonjwa wote bila kujali wala kuangalia vipato vyao ili waweze kutimiza majukumu yao ya kulinda afya ya kila mtanzania.

 
     

Marja-Liisa Swantz  : Wednesday, September 1, 2010    
 

Kwa Martin Mandalu na wanaume wengine.
Wasichana wa umri chini ya miaka 15 hata wasichana wakubwa zaidi hawapati mimba kama hawakaribiwi kwanza na  wanaume na kuwavuta kwa tendo hili. Ninyi wanaume mzungumze jinsi ya kubadilisha vitendo na tamaa za wanaume.
Mtwara ngoma za wasichana za unyago zinachezwa umri mdogo mno. Kwa kufuata mila waliweza kuanza kucumbiana baada ya unyago. Siku hizi ngoma hizi hazina maana.
Bibi Marja Swantz

 
     

Godliving J. Kessy  : Thursday, August 5, 2010    
 

 

Brethren good day!



 Sorry that I have been quit absorbed with "mahangaiko ya maisha haya", here and there to an extent that I have not been participating in many many important topics that have been in our discussions network.  
I am a bit baffled the way we or most Tanzanians including the entrusted elites look at serious problems ravaging their fellow citizens and remain undisturbed!! I have always lay my blames on leadership on all our problems. This is because they the ones expected to guide, lead and pioneer other community members for any meaningful and fruitful venture. Given right leadership with right policies, poverty becomes just a mental attitude. If a leader is committed to work out with his/her people to solve ant societal problem, the results will just be equal (at minimum) the available resources for the same. We are all aware, that any serious MP in his/her constituency has lived and leave a legacy behind of things he/she accomplished while holding that office.

Therefore Policies and Programs be it on Maternal mortality or children mortality have to yield expected results (o.t.r.e) given the vote owners/mandated leadership care their responsibility of ensuring the plan is implemented to the targeted people and resources provided utilized in time and space. The contributions made here are scientifically correct but is the political will en-culture in feeling the necessity to see the mortality's minimized if not eradicated? Our root problem is leadership lacking commitment morally and ethically hence however good the plans can be, no tangible results as we have lost the art of self regulation and accountability. It is not how much we have but what do we do with the little we have.



 Kessy, G. J.



DAR 


 

 
     

Martin Mandalu  : Tuesday, August 3, 2010    
 

Naam,


 kwa hakika kama tulivyoona kuna sababu kadhaa wa kadhaa ambazo zina sababisha vifo vya kina mama wajawazito. Wachangiaji wameongelea huduma dhaifu katika vituo vya afya, zahanati, na hata katika hospitali zetu kubwa. Wengine wameachangia kwenye suala la umbali wa huduma toka kwenye makazi ya wananchi hasa vijijini. Wengine wamechangia suala zima la wito wa uuguzi; kuna madaktari na manesi ambao wana uwezo mkubwa wa kitaaluma lakini wanakosa kujua namna ya kuwa na mawasiliano mazuri na wagonjwa wao. Na kadhalika na kadhalika.

Jambo jingine japokuwa limechangiwa ni suala la vijana wa kike hasa maeneo ya mikoa Pwani kuanza kujihusisha na vitendo vya ngono wangali wadogo. Naam, tatizo hili nimekutana nalo kwa kiasi kikubwa katika wilaya ya Mtwara vijijini.

Wasichana wadogo wenye umri mdogo wa hadi miaka 12 na 13 unakuta tayari wana watoto. Wenye kubahatika kupata watoto ni wachache mno wengi wao hupoteza maisha wakati wa kujifungua.

Tayari kuna elimu inatolewa ili akina mabinti wadogo waendelee kusubiri kushiriki kwenye tendo la ndoa mpaka umri utakapo waruhusu. Kwa kuwa elimu tayari inatolewa basi wadau wengi zaidi wanaofahamu elimu hiyo wajitahidi kujitoa kuwaelimisha jamii hii ya wasichana wenye umri mdogo ili  kupunguza idadai ya akina mama wajawazito wanaopoteza maisha wakati wa kujifungua.


 Mandalu

 
     

Bariki Karosi Kaale  : Thursday, July 29, 2010    
 

Waheshimiwa wadau wa TAKNET

Naomba kumpongeza na kumshukuru Dr. Kida kwa nasaha nzuri alizotoa. Vyanzo vya vifo vya dada zetu ni vingi. Ukosefu wa huduma za afya ni moja wapo - kutokana na umasikini.

Naomba kutoa mchango wa awali na baadae nitatoa mchanganua zaidi. (Paper backed by proven research data). .Baadhi ya tafiti zinaonyesha ukosefu wa nishati ya kupikia na mwanga wa taa vinachangia  kwa kiasi kikubwa vifo vya wamama ambao ndio wanahusika hasa na kutafuta kuni na kupika kwenye mazingira  yenye moshi (in door pollution kitchens). Kwa zaidi ya karne tano  asilimia 98 ya Watanzania wameendelea kutegemea kuni kama chanzo kikuu cha nishati ya kupikia. Upatikanaji wa kuni unapungua na sehemu nyingi miti imetoweka. Serikali haina mikakati ya kuhakikisha kuni za kupikia zinapatikana au nishati mbadada (affordable and relaible alternative energy sources for household cooking). Wakina mama wajawazito na wanaonyonyesha wanateseka siku kwa siku kuokuta kuni. Wanatembea zaidi ya km 10 kwa siku huku wakibeba mzigo wa 25-30 kg wa kuni. kila trip kitendo ambacho kinadhoofisha afya zao.

Utafiti unaonyesha kwamba mwaka 1961 kila Mtanzania alikuwa na wastani wa hekta 7.0 za msitu wa asili na kuni zilikuwa nyingi. Kwa mwaka 2009 kila mtanzania alikuwa na wastani wa 0.7ha za msitu wa asili na kuni zinapatikana kwa shida. . Kwenye maeneo mengi hapa nchini miti mikubwa imetoweka kwa hiyo ardhini hakuna tena mbegu za miti ya asili tuliyozoea ambayo inatoweka kwa kasi kwani haitaweza kuota tena kutokana na ukosefu wa mbegu...


Kuni/mkaa zinachangia asilimia 92 ya nishati inayotumika Tanzania bali ni chini ya asilima 0.3 ya bajeti ya nishati inatumika kuendeleza upatikanaji wa kuni.. Kipau mbele cha maendeleo ya nishati ni umeme ambao hadi sasa ni chini ya Watanzania 600,000 kati ya 42,000,000 wanatumia umeme kwa kupikia. Umeme umepewa zaidi ya asilimia 99.6 ya bajeti ya nishati mwaka huu wa fedha. Pamoja na hizo juhudi nzuri - tatizo lililopo ni kwamba Watanzania walio wengi hawataweza kupikia umeme kwa siku za karibuni. kwa hiyo wataendele kutegemea kuni/mkaa. 

Kutoweka kwa misitu kutokana na kuni - ambazo ni hitaji muhima la kila siku kwa maendeleo ya kaya pia kunachangia uharibifu wa mazingira, hasa uharibifu wa vyanzo vya maji na kufanya maisha ya wakina mama kuwa magumu zaidi.

Kwa maoni yangu juhudi za pamoja zinatakiwa kufanywa na kila sekta kutatua tatizo lililopo. Sekta ya afya ni sehemu tu ya wadau na tunawashukuru kwa mchango wao. Sekta zingine kama nishati, viwanda, elimu, hazina n.k ziwepo.
Bariki K. Kaale ( Mtaalamu wa Nishati UNDP -TZ)


  

 
     

japjet Makongo  : Wednesday, July 28, 2010    
 

Tafiti zimetuonyonyesha kuwa baadhi ya sababu za vifo vya mama wajawazito vinatokana na ukatili wa kijinsia hususani majumbani. Wanawake wanapigwa, kunyanyaswa na kusababishiwa ulemavu wa kudumu na hata kuathirika kisaikolojia. Njia ianyotumika ni kuwalemisha na kuwawashawishi wanaume washirki kikamilifu katika malezi ya ujauzito wa akina mama, ikiwa ni pamoja na kuongozana nao katika vipindi vya kiliniki.


Inawezekana kuna badhi ya wanaume walioanza kuhudhuria klinik na wake zao au wapenzi wao japo kwa kasi ndogo. Kwa sasa ni vigumu kuwajua kwa vile hakuna mfuo unaochukua rekodi zao katika kliniki na vituo vya afya. Kinachotakiwa ni kurekebisha daftari za rekodi za MTUHA ili kuwepo na sehemu ya kujua wamaume wangapi walihudhuria na wapi. Inawekezekan hii ikaonekana kuwa sababu ndogo, lakini nadhani itejenga kivutio kwa wanaume. kazi kwenu wizara ya afya.


Makongo

 
     

Omari Mwinyi Khamis  : Monday, July 26, 2010    
 

I completely agree with Irene Alenga that men can play a big part in this problem.That the  heath care program that takes place at the  Ngaranaro Health Centre in Arusha should actually include men as well. Husbands should follow their wifes in such a training.I remember to follow my wife to th hospital in Sweden when she was pregnant and we were both trained as how to act in different situations.I was also present during the last moment during the birth of the children.


However, there are some complications that require the experience of a nurse or a doctor.Therefore pregnant women have to be advised to visit hospitals ferequently if they detect something is wrong.The medical information is of paramount importance in several pregmant cases and can save serevral lives.


Yes Dr.Tausi Kida there is no nation without people and our politicinans knows this very well.We need to incerse the health budget from 7.74 USD to at least 10.5 USD per year.We must take care of the future generation not only in education but also in health maters.


 


Dr.Khamis

 
     

Dr. Tausi Kida  : Thursday, July 22, 2010    
 

Dear TAKNET members


Napenda kuwashukuru kwa maoni yenu mliyoyatoa mpaka sasa kuhusu tatizo hili la vifo vya  akina mama kutokana na matatizo ya ujauzito. Kwa kweli tatizo hili ni kubwa kote mijini na vijiji , lakini takwimu zinaonyesha kwamba  sehemu nyingine kijiografia zimeadhirika zaidi ya nyingine na hasa sehemu za vijijini. Baadhi ya takwimu kuhusiana na suala hili zinaweza kupatikana katika ripoti ya PHDR 2005, ambako   maternal mortality rates  (MMR) zimeripotiwa katika ngazi ya wilaya.


Katika kutafuta ufumbuzi wa suala hili ( kama  baadhi ya wadau walivyosema)  kunahitajika   kufanyika utafiti  wa  kina  ili kufahamu kiini cha tatizo na pia kuhusisha matatizo mengine   nje ya sekta ya afya  ( other structural problems)  yanayochangia kuongezeka kwa  tatizo hili  mfano  ngazi ya elimu kwa jamii,  mila potofu etc.


Ni vizuri kuzingatia kwamba ufumbuzi wa tatizo hili utahitaji hatua za haraka (immediate measures)  zikihusishwa na  mipango ya muda mrefu.  Serikali   pia inatakiwa kuwa na wito madhubuti hasa katika kutenga fedha kwaajili ya kuboresha huduma za uzazi . Ni muhimu kujua kwamba kwa sasa nchini Tanzania  ni asilimia 15 tu ya  zahanati zina uwezo  kutoa huduma  bora  kwa  masaa 24 kwa mama wajawazito.  Hivyo basi jitihada zinahitajiwa kuboresha vitendea kazi katika kutoa huduma hii  i.e improvement of infrastructure for obstetric care.  Hivyo hakuna  budi kuongeza matumizi ya fedha katika kuboresha huduma hii na kupunguza matumizi mengine yasio na lazima . Je tuko tayari?  Ikizingatiwa kwamba allocation ya pesa za afya kwenda katika ngazi za wilaya imekua ikiongezeka kwa asilimia ndogo sana ( angalia PER 2008). Pia our per capita health spending bado ni ndogo sana 7.74 (USD)  - bajeti  ya asilimia 7.74 kwa mtu kwa mwaka  – katika mwaka 2007/2008 ukilinganisha na target ya WHO ya USD 34 kwa mtu kwa mwaka.  


Pia suala zima la kutoa huduma bure kwa  akina mama wajawazito linatakiwa liangaliwe kwa kina na lisibakie katika sera tu.  Wakina mama wengi bado wanahangaika kutafuta fedha za vifaa muhimu kama cloves  na nyuzi, kulipia huduma za usafiri na chakula pindi wako hospitali , na pia kuwa na  fedha za kutoa asante kwa wakunga n.k  . Hali hii inaleta utatanishi mkubwa kwa wakina mama wakati wanapokwenda kujifungua


Regards,

 
     

Mwisomba Titus  : Thursday, July 22, 2010    
  Ndugu Wa TAKNET,

Naitwa Likanga, nimejiunga jana tu na Mtandao huu na ni imani yangu kuwa wengine wataendelea kuja kwani ni mahali pazuri kwa kupashana habari.

Kwa maono yangu ninafikiri hili tatizo la Vifo vya akina mama kutokana na matatizo ya Ujauzito, linaweza kutatuliwa na wadau wote kwa ujumla, yaani Serikali, NGOs, Wanakaya wenyewe kwa kushirikiana na kuliona kuwa hili ni tatizo. Inawezekana kabisa kama juhudi za kujenga hospitali na kuboresha huduma za afya zikifanywa kwa pamoja (Participatory Approach), tatizo hili linaweza kuwa ni hadithi za kale.

Pia Elimu itolewe kwa wote (Baba, mama na wanafamilia) juu ya umuhimu wa kujifungulia Vituo vya Afya. Akina mama wengine hawawezi kujifungua katika kituo cha Afya kwa sababu Mkunga aliyekuwepo pale ana umri sawa na Mwanae wa kwanza, hivyo anaona heri ajifungulie nyumbani chini ya Mkunga wa jadi ambaye hata hivyo hajapata mafunzo. Kwa hiyo hapa ni swala la "change of mind set". Hivyo ni muhimu elimu shirikishi ikatolewa na Wizara husika kwa kushirikiana na wadau wengine.

Kuwe na mawasiliano ya mara kwa mara kati ya Wakunga wa jadi pamoja na watoa huduma ya afya chini ya Wizara ya Afya, ili kupata mjulisho nyuma wa kile kinachoendelea katika Jamii. Kwa upande wa Serikali ihakikishe inasimamia vyema huduma hizo, isiwe kwamba sheria ipo ya akina mama wajawazito kupata huduma bure kutoka katika vituo vy afya, lakini sheria hiyo haitekelezwi na wale waliopata majukumu ya kuyasimamia. Kwa mfano, gari la wagonjwa lipo, ila ukifika na mama mjamzito unaambiwa gari halina mafuta, hivyo uchangie. Sasa hiyo inaweza kuwa ni tatizo kwa wengi kwani kiasi hicho wanachoambiwa kinaweza kuwa kipo nje ya uwezo wao.

Wapendwa, mimi nimeliona tatizo hilo kwa jicho hilo, lakini bado mwingine anaweza kuliangalia kwa jicho lingine pia.

Asante

Likanga

 
     

Omari Mwinyi Khamis  : Thursday, July 22, 2010    
 

Swala la vifo vya mama maja wazito ni ngumu sana hata kwa chi amazo zimeendelea.Mfano wa mja mzito kucheleweshwa kwa sababu hakuna gloves ni kwa sababu ya kinga yake ili asipate magonjwa kama AIDS wakati wa uzazi.

Jambo muhimu kwa nchi nzima ni kupanua huduma za waja wazito ili waewe kupewa upelelzi wa mimba zao mara kwa mara pamoja na matibabu yanayo hitajika.Mama waja wazito hawatakiwi kufanya kazi za dharubu.Kwa mfano nilpokuwa nafanya kazi katika mgodi Sweden tulikuwa na mwanamke ambaye alikuwa anafanaya kazi ya kuchimba mgodini.Lakini alipokuwa na miba ilibidi tumpe kazi nyingine ambayo haihitaji kutumia nguvu.Tulimpa kazi ya kuchora ramani za mgodi(production unit).

Pia wajazazito wanahitaji kuelimishwa na kufanyiwa uchunguzi mara kwa kwa mara kati ya mwezi wa sita na nane mpaka mwezi wa tisa.Mama wakunga ndio ambao wanayo elimu hii ya kuwasaidia majawazito.Wao wangeliweza kutambaza elimu kwa jamii kwa kutumia vyombao vyote vya harari nchini.

 

Der.Khamis

Sweden

 
     

Bughali Frank  : Thursday, July 22, 2010    
  It is true that maternal motarity is realy a problem in most of all african countries.the cause of this problem is that there is abig gap between health workers and women, so if we creat friendship between this two sides it will reduce the problem.this is because many women fears the abusive laguage used by nurses  
     

IRENE ALENGA  : Thursday, July 22, 2010    
 

I will start my contribution with a preamble. Following reserch that has been done by the UNFPA world wide, maternal and child mortality rates are a big indicator of poverty in any country in the world. Maternal mortality is the largest health inequity in the world; 99 per cent of maternal deaths occur in developing countries – half of them in Africa. A woman in Niger faces a 1 in 7 chance during her lifetime of dying of pregnancy–related causes, while a woman in Sweden has 1 chance in 17,400. With a record of 529 maternal deaths in every 100,000 women in a population of almost 40 million people where does this place Tanzania? Have we not been able to save the lives of our mothers, sisters, daughters, wives because of poverty?


We have all discussed about government interventions but what is our role as individuals? At a nuclear level, what is the husband’s/ faters role in ensuring the safety of the expectant mother? I read with a lot if interest an article in the Daily news published on the 21st July 2010 on how husbands can reduce maternal deaths. If we digress into this perspective they play a very major role to the well being of the expectant mother from conception to delivery and post delivery periods either physically, mentally, spiritually or emotionally. This person spends a susbtatial amout of time with the pregnant woman and would therefore be able to track the development of the pregnancy and be the first engagement point if any complications develop. So while a lot of efforts have been focussed on the women we should not ignore the men. This should be the best point of intervention.


We should specifically target this group of individuals and engage them in pre-natal care training. In western cultures, the responsibility of parenthood is a shared one unlike African culture where there is a clear division of labor for men, women and children where roles are properly defined and strictly followed. I talk in this perspective because most of these deaths are experiencd in rural areas. True to experience given by most of the contributors, access to facilities, properly trained doctors, nurses and midwives or even equipment contribute to these deaths but lets not forget knowledge is power and that’s why we have advocate for First Aid to save lives. It is the first response to any complication in expectant mothers that hangs their balance for survival.


At the Ngaranaro Health Centre in Arusha, there is a training program offered every morning to pregnant women called the “Individual Birth Plan Training” Imagine what a differene it would make if husbands/ fathers also attended this training alongside their partners.

 
     

Festo E. Maro  : Wednesday, July 21, 2010    
  Ningependa kwenda moja kwa moja kwenye mchango wangu kuhusu hii mada kwani waliotangualia wamesha elezea umuhimu na kuiweka mada hii katika mtazamo wa majadiliano. Ni jana tu usiku nilikuwa nasilikiza na kutizama TBC1 ambapo reporter wa Mkoa wa Songea alikuwa anaelezea adha ambazo mama wajawazito wanaendelea kuzipata hata baada ya miaka arobaini ya uhuru. Katika taarifa yake nimeona kuwa uhuru huu ni kwa wengine lakini siyo mwanamke ambaye ni mjamzito. katika hiyo taarifa nilisikia kwenye hiyo hospitali ya mkoa wa ruvuma vipo vitanda 50 tuu katika wodi ya wazazi lakini huwa kuna mama wajawazito walio jufungua na wanaotaka kujifungua kati ya 80 na 100. Daktari alisema inabidi kitanda kimoja kitumiwe na wajawazito wawili mpaka watatu. Hali hii inasababisha kila mama mjamzito aje na msaidizi wake kutoka nyumbani ambaye atalala nae kuangalia mtoto asije kulaliwa au kudondoka chini. Manesi waliopo hawawezi kuwaangalia wajawazito wote kwa ufanisi.
Ukitafakari hali hiyo katika za wodi za wajawazito utaona kuwa msongamano nimkubwa sana. Hali hii ina sababisha matatizo mengine kama hali ya hewa kuwa nzito kusababisha watoto wachanga na mama wajawazito kupumua kwa taabu. vilevile utaona kutakuwa na msongamani mkubwa katika matumizi ya huduma zingine kama vyoo na mabafu.
Daktari wa hiyo hospitali alisema hiyo imekuwepo hapo hospitalini kwa mda mrefu sana na kwa mda wa miaka miwili amekuwa anafuatilia kwa karibu bila mafanikio ya haraka. Maranyingi viongozi huwa wanajitetea kwa kusema fedha hazipo kukidhi mahitaji ya kuboresha wodi za wajawazito. Lakini chakushangaza wabunge walidai nyongeza za mishahara yao bila hatakufikiria kiasi hicho cha fedha kingeweza kuleta tofauti katika sehemu mbalimbali hapa nchini.
Kuna haja ya kuweka vipaumbele kwenye maeneo ambayo ni muhimu hasa miundombinu ya kuwahudumia mama wajawazito ili kupunguza vifo na taabu wanazozipata.
 
     

Angomwile Fungo  : Tuesday, July 20, 2010    
 

Tatizo linaweza kuwa kubwa kuliko vile linavofikiriwa, kwa sababu kuna wale walioko vijiji vya ndani ndani kama Lendikinya(Monduli) ambako upatikanaji wa data ni karibu na hamna.

Sababu ya Vifo,

  • Kuchelewa kufika hospitalini/dispensary.

  • Mimba katika Umri mdogo.

  • kwa wale wanao wahi hospitalini, uzembe wa wakunga(hasa hospitali za serikali).

  • ukosefu wa elimu ya uzazi (hasa vijiji vya ndani ndani na kiasi mijini) kwa wakunga na wazazi watarajiwa pia.

Napendekeza,

  • Uzembe wa Wakunga. Apo ndio kuna balaa kama nini. SULUHISHO, linahitaji mipango ya kudumu na muda mrefu_kuelimisha wakunga kuhusu umuhimu wa kazi yao kwa jamii, kuboresha maslahi yao, na kuelimisha jamii kuhusu haki zao za kiafya. Uwepo usimamizi (kama vile audit ivi). na kuwaondoa wale wanaobaininka kuzembea.

  • Kwanza kuwe na utashi wa kisiasa, kiuchumi, na kijamii tokea chini. yaani kuanzia na wazazi watarajiwa wenyewe, wanasiasa na watendaji serikalini. hii inasaisia kuleta PRESHA ya mabadiliko ya lazima kama kutenga bajeti ya kutosha kwa ajili ya mambo ya uzazi kuanzia na familia mpaka serekelini.

  • Miundo mbinu iboreshwe

  • Jamii hususani wazazi watarajiwa wale vijana wanaotoka utotoni kwenda utu uzima wapate elimu ya kutosha kuepusha mimba katika umri mdogo.  elimu hii itolewe mashuleni, misikitini, makanisani yaani mahali popote ambapo watu wenye nia moja hukusanyika mara kwa mara.

  • elimu ya ukunga  wa jadi iendelezwe na kuboreshwa.
 
     

Grace Millinga  : Tuesday, July 20, 2010    
  Napenda kuanza kwa kuwashukuru taknet kwa mada nzuri mliyotoa.
Kwanza napenda kumuunga mkono Mr.Adolph Massawe,
 Kwa kweli this is a big problem kwetu Tanzania and other developing nations,linaumiza na linamaliza ndugu zetu ambao ni wajawazito na hasa hawa vichanga ambao hupoteza maisha either kwa huduma mbovu aipatayo mama au kutokuwepo kwa huduma za afya karibu.
Mimi kwa upande wangu nahisi ufumbuzi wa tatizo hili ni kuhakikisha huduma za mama wajawazito zinaboreshwa ikiwa ni pamoja na madawa,vifaa,usafi na uangalizi wa karibu wanapokuwa wodini.Nasema hivi kwasababu ni siku nne tu zimepita tangu dada yangu ajifungue na nilipokuwa hospitali nilishuhudia mama mjamzito alicheleweshwa kupewa huduma eti kwasababu hakukuwa na gloves.
 
     

david masambe sando  : Tuesday, July 20, 2010    
 

Napenda kutoa maoni yangu pia katika hili kwani limenigusa pia !



Ni kweli kabisa, ukiwa kwenye huduma ya tiba utagundua hospitali zina asilimia fulani kwenye kuchangia haya, hata hivyo mambo mengi yanachangia tena kwa aslimia kubwa,



Ni mambo mengi sana ikianzia elimu ya mzazi, miundombinu ya kumpeleka mama hospitali, uwepo wa karibu wa vituo vya afya na mengine mengi. Kwa ukweli vifo vya akina mama vinavyotokea mahospitalini mara nyingi ni mama kufika akiwa amecheleweshwa na yuko katika hatua mbaya sana, ingawa sisemi kwamba kuna ambavyo wahudumu wanachangia na mazingira ya kazi.



So vifo vingi ni michango ya mambo mengi ambayo hata ukiwa na hospitali kote nchini na karibu na wananchi, kama maendeleo bado chini na elimu ni duni havitaisha, tatizo nimfumo mzima wa maisha na huduma za jamii



Tuangalie kwa mapana zaidi



regards

 
     

Kamala Lutatinisibwa  : Tuesday, July 20, 2010    
  Nacnhangia hapa nikiwa nimetoka kupata mtoto siku mbili zilizopita. niliilazimika kuachana na hospitali ya mkoa wa Bukoba kwa uuzoefu wa waliotangulia kupaa huduma pale na hivyo kulazimika kumpeleka mke wangu hosp ya misheni na ya wilaya ya missenyi ili kuapata huduma, sikuamini kuwa niliambia napaswa kulipia shs 1,500 tu kwa siku zote mke wangu alipokaa pale lakini pia huduma zilikuwa nzuri. japo mimi sio mpenzi wa siasa lakini nafikiri hii nihatua kuubwa ya kuokoa maisha ya wazazi na watoto.

Ila changamoto zilizobaki ni kama vile usafiri wa kupelekwa hao wakazi wa vijijini hosp. kwa mkoa kama kagera wamejitahidi kwamba bara bara zoote zinapita kwa kiasi. ila sasa umasikini wa wazazi kupata usafiri wa kuwawaisha inabidi uangaliwe upya

Tunahitaji juhudi za makusudi, kwa mfano kuwezesha wazazi kuishi karibu na hosp au karibu na usafiri waonapo siku zimekaribia.  kuajaribu kujitengea pesa waonapo siku zimekaribia na kuka makini muda wote
 
     

EUSEBIO J. CHILIPWELI  : Tuesday, July 20, 2010    
 

Mimi mchango wangu ni mdogo tu. Ningependa kwanza tatizo hili kwa jinsi lilivyo liainishwe kwa misingi ifuatatyo na ndipo tuanze kutatfuta njia za kulikabili:



1. Jinsi tatizo lilivyo kwa wakazi waliopo mijini ambako huduma zipo karibu, ni kiasi gani au kwa kiwango gani tatizo hili lipo!



2. Kwa kiwango gani tatizo hili lipo vijijini ambako diko waliko akina mama wengi walio mbali na huduma za afya.



3. Mila na desturi zinachangia kwa kisai gani kubaki au kukua kwa tatizo hili, na ni maeneo yapi yenye kugubikwa zaidi na tatizo  hilo na kuhitaji msukumo wa pekee katika kulikabili.



4 Kutokuruhusu tatizo hili liedeshwe kisiasa badala ya kutumia takwimu na hatua madhubuti kulikabili.



Kwa maoni yangu swala hili limo midomoni mwa wanasiasa wetu kila wanapotafuta umaarufu kwa wapiga kura wakati wanapowahitaji wawape "ulaji". Wakisha pata ulaji hawana tena nafasi ya kuangalia yanayowasibu waliowapa ulaji, hasa akina mama ambao ni ndio wapiga kura wengi.



Ni muhimu kuainisha ni vitu gani vinavyoletea 'maternal motality'



katika mazingira yapi ( mijini na vijijini) ndipo tuone jinsi gani tunaweza kukabiliana navyo. Nani afanye kazi hiyo?



Labda niachie mchango wangu kwa sasa hapa ili wenzangu tupate nafasi ya kuuendeleza.



E.Chilipweli.

 
     

Gideon Karuguru  : Tuesday, July 20, 2010    
 

Naomba nijitambulishe kwa wan TAKNET kwamba mimi ni mdau mpya naitwa Gideon Mabanga Karuguru.
 
Awali ya yote napenda kuungana na wachangiaji waliotangulia na pia kuwapongeza kwa michango yao. Kutokana na uchangiaji huu tunapata picha kwamba tunao watu, wanaoelewa na kuugua kutokana na utendaji mgando ulioko katika mfumo wetu na serikali, baadhi yetu tukiwa humo humo ndani na pengine kutokana na mazingira yaliyopo tumeshindwa kufanya mabadiliko.
 
Niungane na Apronius Vitalis Mbilinyi katika baadhi ya vipengele kwa kuchangia ifuatavyo:
 
Suala la vifo vya akina mama kutokana na matatizo ya ujauzito (Maternal Mortality) huwezi kulizungumza kwa kulitenga na vifo vya watoto wachanga (Infant Mortality) na hivyo linachukua sura pana zaidi ya namna linavyoonekana. Changamoto kubwa inayotukabili sisi kama nchi inatokana na namna tunavyofikiri, kupanga na aina ya watu ambao tumewapa dhamana ya kutengeneza mipango yenyewe na kuweko kwa siasa zisizo halisia.
 
Nianzie na suala la watumishi: kwa wakati tuliomo Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inatekeleza Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM) na ndiyo msingi mkubwa wa 'sera' ya zahanati kila kijiji na kituo cha afya kila kata. Binafsi si muumini wa 'sera' hii kwa sababu naamini katika kuchapa kazi kwa bidii, uaminifu na umakini ili kupata matokeo yaliyo bora. Naomba nikariri msemo kutoka gazeti la Majira J3, kwamba 'maisha bora hayawezi kuja kwa kucheza pool'. Ni kama vile tunacheza pool, tunachezea pesa, tunapoteza mchezo mmoja baada ya mwingine wakati huo huo tukiota kujenga nyumba na kuishi maisha mazuri ilhali kazi hatufanyi. Naomba nirudi kwenye mada.
 
Mojawapo ya malengo makuu katika MMAM ilikuwa ni kuzalisha wataalam wa kutosha ili waingizwe katika ajira ya umma na kusaidia kuboresha ubora wa huduma inayotolewa na zahanati na vituo vya afya. Batch ya kwanza ya wataalam wa kada za utabibu na uuguzi kwa ngazi ya cheti imetoka mwaka jana mwishoni na mwaka huu mwanzoni, wengi hawajaajiriwa kwa sababu hakuna vibali vya ajira kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi, kwa sababu Hazina haikuwa na pesa ya kutosha kwa ajili ya mishahara, kwa sababu mapato ya Serikali na hasa makusanyo ya kodi kutoka TRA yameshuka na pesa haitoshi, kwa sababu watu wengi hatulipi au tunakwepa kulipa kodi, kwa sababu ...... wenzangu mwaweza kuendelea kunyumbulisha.
 
Ukiacha wataalam hawa wa kada za chini ambao hawajapata ajira, tuangalie ajira ya madaktari wanaofuzu kutoka vyuo  vyetu vikuu, kwa sasa tunazalisha takribani madaktari 600 kwa mwaka (mwenye takwimu nzuri atanisahihisha) lakini kwenye ajira ya umma wanaingia wastani wa 200 kwa mwaka, wanaobaki wanatafuta pa kwenda, baada ya kuwa tumewapa grant ya kusomea taaluma hii muhimu, wanachukuliwa na wengine. Je, tuna nia makini kweli ya kupunguza matatizo yetu?
 
Ukiwasikiliza waheshimiwa wanazungumza wanakiri kwamba huduma zetu za afya zinatolewa na watu wenye utaalam wasiozidi 40%, maana yake tuna pengo la 60% kufikia viwango vya kimataifa, kama ndivyo, je tunahitaji vibali kuajili wataalam tuliowaandaa sisi wenyewe kwa gharama zetu na wakati huo huo tukitambua kwamba kuna wataalam wanastaafu na kufa kila siku inayopita? Je tunahitaji kweli kuongeza majengo ya zahanati na vituo vya afya wakati vilivyopo havina wataalam? Tunahitaji zaidi maamuzi na kuwa wa kweli.  

 
     

jason nkyabonaki  : Tuesday, July 20, 2010    
  Napenda kutumia nafasi hii kuwapongeza kwa kuamsha mawazo namna ya kuzuia vifo vinavyotokana na uzazi.Mimi najielekeza kwenye nadharia ya kiutamaduni(cultural relativism theory).Dhana kubwa hapa ni kwamba kabla ya hospitali hizi tulizonazo leo,tulikuwa na mfumo wa tiba za asili na ambazo zilifanya kazi vizuri.Wanawake wajawazito walikatazwa vyakula fulani fulani kama mayai wakiambiwa mtoto angezaliwa bila nywele,nakadhalika.
Pili,tulikuwa na dawa za kiasili ambazo wakunga wa jadi waliweza kutoa na akina mama wakaweza kunywa na kujifungua salama.Leo hii,ni mama yupi atakubari kunywa hizi dawa kama si kwenda hospitali na ambazo zimesongwa na matatizo mbalimbali lakini pia ambazo zinaweza zisitusaidie kwa maana kama kule Kagera watu husema kuna magonjwa ya kwenye kitovu(inherited diseases)ambayo hata hospitali wanaweza wasiwe na dawa lakini wao hujua historia ya ukoo katika mfumo wa uzazi.

Kutokana na mawazo hayo mimi nahisi suluhisho tufikirie upya tiba yetu ya asili na hii ndo motto tunaoita(African Renaissance).Hivyo basi turudi na sisi wenyewe tuboreshe kiwango cha tiba zetu za asili kwa kuwatumia bibi zetu kupata tiba ya asili.
Tukumbuke hatutapoteza tena maisha kama tukirudia kile ambacho tumekipoteza kwa kuambiwa ni kibaya au ni uchawi ili huyo mtu atumie mti huohuo aukaushe na akwambie usafiri kilometa 1000 kufuata mahali panapoitwa hospitali badala ya kufuata kwa mama Koku ambaye yuko mita 100 tu.

Nafikiri tujielimishe na tubadili attitude zetu kwa kile Thiongo anachoita "Decolonization of the mind" tukifanya hivyo tutapiga hatua na vifo vitokanavyo na uzazi itakuwa historia na tunaweza kuwa msaada mkubwa kwa taifa na bara zima la Afrika.

 
     

Dorah Semkwiji  : Monday, July 19, 2010    
  Aksante sana TakNet kwa kutupatia tena nafasi hii ya kuchambua mada mbalimbali zinazoelezea mustakabali wa watanzania. Napenda kushukuru kwa mada hii ya vifo vya akina mama na ongezeko lake kila kukicha licha ya jitihada zinazoonekana kufanywa.

Ninaungana kabisa na wachangiaji waliotangulia. Kusema ukweli ninapolifikiria hili suala mimi huwa kidogo naona kama bado jitihada za lazima au tuseme msisitizo wa lazima katika kutatua tatizo hili hazijafanywa kikamilifu. Nina imani kabisa na serikali yetu kuwa ikiamua kushughulikia jambo inaweza kabisa tatizo tu ni wapi tunapoweka priorities zetu. Tukiangalia priorities zinazowekwa katika nchi yetu kwa kweli nyingi huwa zinalenga katika kuukuza uchumi wa nchi yetu. Najua kuna watakaosema kuwa uchumi wa taifa ukikua basi na huduma nyingine zitaboreka ni kweli lakini tusisahau pia umuhimu wa ugawanywaji ulio sawa wa hayo maendeleo kwa sababu nchi inawezakuwa na uchumi mkubwa lakini ukamilikiwa na wachache -huku ukiwaacha wengi wakiwa na hali duni kiasi cha kuwafanya wakose huduma muhimu za maisha. The same applies katika level ya kitaifa kuwa tunawezakuwa na uchumi uliokuwa lakini ukaishia katika kuboresha sehemu tu ya huduma za jamii mf. elimu na kuzisahau nyingine au hata kutoa uwiano usio sawa.

Nikiiangalia hali ya huduma za kina mama ninajiwa na mashaka kana tutawezakutimiza lile lengo la milenia juu ya kupunguza vifo vya akina mama wajawazito. Nafikiri serikali yetu inatakiwa itilie mkazo sana juu ya hili na pia iwepo sheria ya kuadhibu wauguzi wazembe ambao kwa namna moja au nyingine huchangia sana katika vifo hivi. Ni mara nyingi tumesikia vifo vya kizembe na kuishia kusema ni bahati mbaya au siku yake imefika ilhali aliyesababisha uzembe anabaki akichukulia kuwa ni busness as usual kiasi kwamba hata kesho akifanya mwingine ataona sawa tu bila kujali kuwa maisha ya binadamu yakipotea hakuna cha kufidia kwa familia iliyopotelewa.
 
     

cecilia valla  : Monday, July 19, 2010    
  Nakuunga mkono Khalfan- na iwapo TOR ita tengenezwa, tunaweza kuona vile tuta saidiana kutatua MMR yenye iko juu sana Tanzania- currently 558.

If anyone has any documents to show the high MMR in various parts of Tanzania tafdhali please send to me.  cecilia.valla@worldvision.com.au

Thanks,
 
     

Adolph massaswe  : Monday, July 19, 2010    
 

Asante kwa swala la msingi la vifo vya wanawake wajawazito.
Napenda kutoa mchango wangu hapa naona yafuatayo yawekwe wazi kwa watanzania:
1. Watu waelimishwe vya kutosha kuhusu mimba za utotoni
2. Wakinamama waelimishwe (kiliniki) wakiwa wajawazito waelewe undani na dalili mbaya zinazoweza kutokea
3. Serikali itoe huduma za karibu za kijamii mfano hospitali ziwe karibu na makazi ya watu
4. Pia kuhakikisha kuwa usafiri ni bora ukizingatia barabara ili mamamjamzito aweze kufika hosp mapema
5. Kuwapa moyo hata wakunga wa jadi ambao hutoa huduma ya kwanza kwa maeneo yasiyokuwa na hospital karibu
        Nafikiri tukiangalia hilo swala kwamtazamohuo tunaweza kupata na mawazo mengi mapya yatakayotusaidia
asanten

 
     

Khalfan Salim Suleiman  : Monday, July 19, 2010    
 

to me nahisi hii ni jambo zuri sana kujadili lkn katika jitihada za kutafuta ufumbuzi wa tatizo hili kwanza ni vyema tukaka chnini na kuangali tatizo liko wapi na linasababishwa na nn  ili tupate kuja kiini cha matatizo hivyo basi we need to carry out /conduct need assessment of maternal mortality this will produce various informatyion with base line subsequently will result into developing sort of strategic plan withj operational plan that inlcude strategic objectives for fighting against maternal mortality.


tukiweza kuona wapi tunamapungufu ndio tunaweza kupanga mpango madhubuti na makakati kwa kupambana na suala hili ili tuweze kufikia lengo kwani mm nahisi niwaombe saaana wataalamu wa afaya kushirikiana na wataalamu wengieo yaan other stakeholders to kuundertake assessment ya issue hii na baadae ku come up with action plan and finaly to develop strategic document for fighiting against marternal mortality.


Hivyo Muhimbili andaeni ToR for the assessment in order the stakeholders and other intersted persons to participate for kwa hivyo natoa wito kwa umma tusaidiane kenwye hili ili tuwe na focus na sio  tuende to bila na pakuanzia na vil vile tuwashajiishe Donors countries to support the effort hata hivyo kila mdau wa hili atengezewe uwajibikaji wake.

 

Wizara ya Afya awajibika kivyake na wengineo ili tupate collective effot

 
     

Dr. Tausi Kida  : Friday, July 16, 2010    
 

Wapendwa TAKNET members,


 Tunapenda kuchukua nafasi hii kuwakaribisha tena  wote kutoa maoni yenu kuhusu mada  hii mpya VIFO VYA AKINA MAMA KUTOKANA NA MATATIZO YA UJAUZITO (MATERNAL MOTALITY) NI TATIZO KUBWA TANZANIA. NINI KIFANYIKE KUTATUA TATIZO HILI?

 
Madhumuni makubwa ni kupata maoni yenu kuhusu jinsi ambavyo serikali na wadau wengine wanavyoweza kusaidia kuondoa hili tatizo. Ukizingatia kwamba kati ya wanawake 100,000 wanawake 578   wanafariki dunia  kutokana na matatizo ya ujauzito (THDS 2004) . Mbaya zaidi pamoja na jitihada zote zinazofanywa na serikali na wadau wengine  tatizo hili limekuwa likiongezeka badala ya kupungua.


Maoni yenu ni ya muhimu sana katika kupatia ufumbuzi wa haraka tatizo hili ; kwa maelezo zaidi tafadhali soma utangulizi hapo juu

Karibuni sana, Moderator: Dr Tausi Kida  na Dr Riziki Ponsiano


 

 
     

  This topic has been closed. You can only view comments!  
     

 

 

  ESRF
  Tanzania Development Gateway
  Tanzania Online
  Government of Tanzania
  United Nations (UN)
More»
 
v  
v TOP CONTRIBUTORS
  Omari Mwinyi Khamis(156)
  Festo E. Maro(69)
  Abdallah Hassan(49)
  japjet Makongo(30)
  Kabuje Furaha(26)
   
All Contributors»



 
Tanzania Knowledge Network (TAKNET) Platform is supported by The Government of United Republic of Tanzania,
United Nations Development Programme (UNDP) and coordinated by Economic and Social Research Foundation (ESRF).


Disclaimer | About Us | Feedback | Membership | Contact Us | Admin
© 2015 Economic and Social Research Foundation. All Rights Reserved.